Wananchi waua majambazi wenye AK 47 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi waua majambazi wenye AK 47

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 30, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa na wananchi baada ya kukutwa na silaha ya kivita aina ya AK 47 na risasi 424 na maganda 14 katika Kijiji cha Sirori, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema tukio hilo lilitokea Desemba 27, mwaka huu saa 2 usiku ambapo majambazi hao waliokuwa wanne wakiwa na mabegi yao, walifika kijijini hapo na kwenda
  kupanga vyumba katika nyumba ya kulala wageni ya Kauli ambapo wananchi waliwatilia shaka na kuanza kuwafuatilia.

  “Baada ya kuingia kijijini hapo, wananchi waliwatilia mashaka na walianza kuwafuatilia hadi pale gesti na walianza kuwahoji, kwa kuwa walibabaika na kutetemeka wananchi hao walichukua mabegi yao na kuanza kuyafanyia upekuzi,” alisema Kamanda Boaz na kuongeza: “Lakini waligundua kuwa kuna mfuko mwingine chini ya kitanda na walipopekua, walikuta silaha moja aina ya AK 47 ikiwa imefungiwa hirizi kwenye mkanda wake, risasi 424 na maganda ya risasi 14.

  “Ndipo wananchi waliamua kupiga yowe na kukusanyika kisha kuanza kuwashambulia kwa kuwapiga na kusababisha vifo vya hao wawili.

  Mmoja alifanikiwa kukimbia na mwingine alijeruhiwa vibaya na yupo mahututi katika Hospitali ya Mkoa wa Mara, alikolazwa kwa ajili ya matibabu,” alisema Kamanda Boaz.

  Kamanda Boaz alisema Polisi inaendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini majina yao, matukio mangapi wameshiriki na akina nani wanashirikiana nao ili kusambaratisha mtandao wao wa uhalifu.

  Katika tukio jingine, lililotokea usiku wa Desemba 25, mwaka huu, Nyangweso Nyamkindo (63) mkazi wa Kijiji cha Nyegina Susebano, Kata ya Kurukerege, Musoma Vijijini alikutwa
  amejinyonga chumbani chake.

  Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu wanadai kuwa kabla ya kufikwa na mauti, Nyamkindo na mkewe aliyejulikana kwa jina la Wagoro Eunyo, walikuwa na tofauti ambazo ziliwapelekea kulala nyumba tofauti.
   
Loading...