Wananchi wanataka Vyombo vya Habari vichunguze vitendo viovu vya serikali

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Watanzania wametoa wito kwa Vyombo vya habari nchini viisaidie nchi kwa kuchunguza vitendo viovu vya serikali yakiwemo masuala ya rushwa na mengineyo.

Nimependezwa na maoni haya ya wananchi. Kwa sababu kama ambavyo Rais John Magufuli anajipambanua kupambana na rushwa, ni vyema wajibu huu ukawa shirikishi kwa maana ya wadau muhimu wa habari ambao wanaweza kufanya uchunguzi na kupata taarifa za matumizi mabaya ya fedha za umma kisha kuyaaniki ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watumishi wasio waaminifu.

Rushwa ni adui.. Adui mkorofi kwelikweli.. Palipo na Rushwa hakuna Haki!

Tupambane..

2.JPG
 
Tatizo la Wanahabari wetu wengi wao wana bei tena very cheap (mnisamehe ndugu zangu)..

Namkumbuka jamaa mmoja wa Kenya anaitwa MOHA wa Jicho Pevu.. Yule Mohammed Ali ni Mwandishi haswa!

Tunahitaji waandishi wa namna ile.. Jerry Muro alijaribu..
 
Back
Top Bottom