Radhia Sweety
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 4,433
- 1,772
Makaidi bwana
We Mmawia Vp?Wananch Wenyewe Hawamtak We Unasema Ndoto Za Alinacha Halafu Ukiitwa Mpumbavu Na Lofa Unalalamika
Hivi UKAWA hawawezi kubadilisha mgombea wa hilo jimbo fasta. Au sheria ya uchaguzi hairuhusu?
kwa hiyo?
Pale pale Duni alimtambulisha yule wa CUF.
Mkuu, ahsante kwa kuleta uzi huu. Ila tukio hili limetokea jana pale Masasi wakati Juma Duni Haji alipohutubia makumi ya wananchi wa mji wa Masasi akimuombea kura Mgombea Urais, Edward Lowasa. Mara baada ya kunadi sera za UKAWA, Babu Duni alimsimamisha Makaidi ili kumuombea kura. Baada ya kusimama, wananchi walianza kumzomea na kuporomosha maneno makali kuashiria kuwa hawamtaki.
Watu hao walipaza sauti zao wakisema kuwa hawamtambui Makaidi kwa vile si mtu wao. Wakasema kuwa asimamishwe Kundambanda ambaye wanaishi naye kila siku na wanamfahamu. Kundambanda amechukua fomu kugombea Ubunge jimbo la Masasi kwa tiketi ya CUF. Baada ya tafrani hiyo, mkutano huo ulivunjika na mzee Makaidi jasho lilikuwa linachuruzika hasa kwapani kutokana na kuhemwa na kile kilichomtokea.
Hapa ni dhahiri kwamba Makaidi Ubunge ameukosa. Ajipange kivingine. Na ni dhahiri pia kuwa UKAWA wameshapoteza jimbo la Masasi Mjini