Wananchi wagawana ekari 30 za Sumaye huko Mabwepande. Asema hana wasiwasi...

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,491
Wananchi waliobomolewa makazi yao maeneo mbalimbali jijini Dsm wamegawana ekari 30 za aliyekuwa Waziri Mkuu awamu ya tatu Fredrick Sumaye. Nae asema hana wasiwasi kwani ana vibali halali vya umiliki.

Chanzo: magazetini
 
Kauli hii ya kuwa hana wasiwasi ni kama anamaanisha ekari 30 zilizochukuliwa ni kapunje tu wamechuku kwakuwa alijimilikisha ardhi kubwa wakati wa utawala wake.
 
Wananchi waliobomolewa makazi yao maeneo mbalimbali jijini Dsm wamegawana ekari 30 za aliyekuwa Waziri Mkuu awamu ya tatu Fredrick Sumaye. Nae asema hana wasiwasi kwani ana vibali halali vya umiliki.

Chanzo: magazetini
Eti nae huyu ni Great thinker...
Ptuuuuuu
 
Mwezi uliopita wananchi walivamia eneo la daniel yona, liko eneo la mapinga bagamoyo ekari zaidi ya 500.

Wakajigawia, watu walikua wanaitana kumiminika kujichukulia ardhi, wakiulizwa wanasema ardhi haijaendelezwa Magufuli hatakubali, watu wakatoka Dar, Morogoro, Chalinze, Tanga na maeneo jirani kujigawia ardhi ya bure.

Baada ya kama wiki 2 kilichowakuta hawana hamu, wengine walijikuta wanakimbia hadi Kibaha kwa mguu, wengine Msata, wengine wakajikuta wanatokea Chalinze kwa miguu.

Wengine wako mahakamani kwa kosa la kuvamia ardhi inayomilikiwa kihalali kinyume cha sheria.

Hata hao wa Mabwepande tusubiri tu tutaona kitakachowakuta.
 
Wananchi waliobomolewa makazi yao maeneo mbalimbali jijini Dsm wamegawana ekari 30 za aliyekuwa Waziri Mkuu awamu ya tatu Fredrick Sumaye. Nae asema hana wasiwasi kwani ana vibali halali vya umiliki.

Chanzo: magazetini

Kwa mtindo huu Tanzania inaingia vitani muda si mrefu. Hakuna sheria ni mabavu. Kama haya mambo yanaruhusiwa na serikali, basi hakuna maana wala sababu ya kuwa na serikali. Tanzanai inakwenda kuwa shamba la wanyama pori, mwenye nguvu ndiye anayesurvive.

Watu wanunue Bunduki na silaha mbali mbali za kujinda dhidi ya uonevu wowote. Hakuna serikali iayolinda na kusimamia haki za raia. Kilichopo ni genge la kulinda watawala na kulilpa visasi.

Serikali itoe tamka kali. La sivyo, serikali inapaswa kukumbuka kwamba binadamu akiwa mjinga kama waTz, hayuko mbali na asili yake ya unyama. Akibambwa auliwe lakini akichance kazi moja.

HII NDIYO TANZANIA TUNATAKA?
 
Back
Top Bottom