Wananchi wa Vunjo wajitoa kutengeneza barabara

malema 1989

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
1,323
Reaction score
530
wananachi wa vunjo wanaoishi mikoa mbali mbali hapa nchini wameungana kwa pamoja na kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe katika kata yao iliyogharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni themanini (80,000,000).Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na wananchi wengine badala ya kulalamika na kuitegemea serikali kwa kila jambo!

Chanzo: TAARIFA YA HABARI YA SAA MBILI JIONI ITV LEO 02/01/2013
 
Wananchi wana haki ya kulalamika wao ndio walipaji kodi, ikiwa serikali dhaifu imeshindwa basi hakuna budi wananchi wakajifanyia wenyewe mambo yao huku wakijua kuwa nchi yao haina serikali inayojali maendeleo ya nchi. Dhaifu anazidi kuaibika na serikali yake ya kifisadi iliyoshindwa kusimamia rasilimani za Watanzania. Sitoshangaa kila mkoa ukitaka kujitegemea kwa rasilimali zake bila ya kuingiliwa na serikali ya kifisadi
 
Twaweza.
Yawezekana ni matokeo ya uchechemuzi na uraghabishi wa Lyatonga Mrema au wameamua tu wenyewe. Kama siyo wao mimi, kama siyo mimi wewe. Twaweza.
 
Hao walishajua kodi zao zinatumika kwenda kubembea majuu hivyo ni lazima wajitegemee. kwa sasa wakusanye kodi na kufanya maendeleo kwenye eneo Lao. hakuna haja ya kuhangaika na serikali fisadi ya kikwete. Kila jimbo lisimamie mapato na matumizi take. tujofunze kuachana na serilali feck za wezi kwani kikwete ni janga la Tanzania.
 
vunjo vijiji gan? Uchira, Kawawa, Karamsingi, Mabungo, Mandangeni, Kirua, Uparo au wap?
 
Wilayani Marangu...no maswali mengi kwakuwa nimeita Marangu wilaya..just wait and see.
 
Wananchi wana haki ya kulalamika wao ndio walipaji kodi, ikiwa serikali dhaifu imeshindwa basi hakuna budi wananchi wakajifanyia wenyewe mambo yao huku wakijua kuwa nchi yao haina serikali inayojali maendeleo ya nchi. Dhaifu anazidi kuaibika na serikali yake ya kifisadi iliyoshindwa kusimamia rasilimani za Watanzania. Sitoshangaa kila mkoa ukitaka kujitegemea kwa rasilimali zake bila ya kuingiliwa na serikali ya kifisadi

mkuu mzalendo mtwara walishaanza, sasa hatudanganyiki!
 
Kumbe wamejitolea hawajajitoa!big up Vunjos
 
kuna wale wanaolaumu wachaga na kujiuliza kwanini uchagani ni kuzuri sasa naona majibu yamepatikana wachaga wanakumbuka kwao, mikoa mingine tuige sio tunajenga maghorofa mijini viijijini kwenye asili yetu tunabaki na nyumba za tope.
 
Back
Top Bottom