Wananchi wa UKONGA tuungane kuhusu usafiri wa Treni

Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,872
1,206
Wanajamvi nikiwa kama mkazi wa jiji la Daressalaam jimboni Ukonga, nakwazika sana na adha ya usafiri wa kutoka huku kuelekea katakati ya jiji!!

Wakati tunategemea zaidi daladala kama usafiri mkuu na ambao haututoshi kabisa, tungeweza kutumia Train ya reli yakati itokayo katikati ya jiji kuelekea mikoani kupitia Pugu jijini Dsm!

Shukrani kwa mh Mwakyembe aliyeanzisha usafiri wa train jijini lakini sielewi ni kwanini usafiri huu hakuna trip ya PUGU~CITY CENTER hali kuna miundombinu ya kutosha na ya uhakika kuliko hata ile ya CITY CENTER~UBUNGO!!

Kwa hisani yenu wahusika na wana UKONGA wote, wakazi wa Chanika, G/mboto, Pugu, Kisarawe,Kitunda na maeneo yoote ya kandokando mwa reli hii shime tuungane kuitaka serikali yetu pendwa ituondolee adha hii kwa kuwa INAWEZEKANA!!
 
Mbunge wetu anawaza kutoka bungen hata umeme sehemu nyingi haujafika kama mbondole, kigezi chini na kivule umeme hakuna barabara shida, sijui waitara anaongeaga nn bungen jaman na hiyo tren ndiyo kabisa hana hata wazo.
 
Kwa Mbunge mimi sina lawama naye kwani wapo waliokuwa na wabunge huku tangia UHURU na wametuacha wana Ukonga kama tulivyo!!

Sasa huyu Waitara wa miezi mimi siwezi kusema kwa kweli, naogopa UNAFKI!!
 
Kaka Magufuli nilimsikia wakati wa Kampeni zake pale Jangwani akizungumzia barabara ya kutoka BANANA~KIVULE~MSONGOLA lakini sioni dalili mpaka sasa mipango ikoje, hii ni mojawapo ya barabara kuu za jimbo hili na nikama haijawahi guswa tangu ivumbuliwe!!

Labda tuseme bado ni mapema kwa utawala wake lakini wana Ukonga tungependa nasi tutembee kwenye barabara nzuri tutokapo makwetu, na tujihisi tunapata mgao wetu kwenye keki ya taifa!!
 
Back
Top Bottom