WANANCHI WA kWEMBE HAWAJALIPWA STAHILI ZAO

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
MGOGORO wa ardhi baina ya wananchi wa eneo la Kwembe Kati, katika Kata ya Kibamba wilayani Kinondoni, na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, umechukua sura mpya baada wananchi hao kutinga katika ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutaka aumalize.
Wananchi hao walikwenda katika ZA PINDA kwa lengo la kuonana na Waziri mkuu,ili kufikisha kilio chao kuhusu kile walichokielezea kuwa ni uonevu wanaotendewa na maofisa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Hatua ya wananchi hao kubisha hodi ofisini kwa Waziri mkuu, inafuatia tangazo lililotolewa na wizara hiyo ya Ardhi Nyumba na juzi likieleza kuwa utaratibu wa upimaji wa viwanja katika eneo la Kwembe Kati, umekamilika.
Tangazo hilo lililotolewa kupitia katika vyombo vya habari, pia liliwataka wananchi wenye mashamba au nyumba zinazopitiwa na njia za miundombinu, kuripoti wizarani kabla ya Januari 19 mwaka huu, kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kununua viwanja hivyo.
Taratibu hizo ni mapoja na kujaza fomu maalumu na kukamilisha malipo ndani ya wiki mbili.Hata hivyo jitihada za wananchi hao kumuona Waziri mkuu, hazikufanikiwa kwa kuwa yuko likizoni.
Badala yake malalamiko yao yalipokelewa na Ofisa wa Kitengo cha Siasa na Bunge (Malalamiko), Consolanta Njalamoto.
Habari zilizopatikana katika kikao baina ya wawakilishi wa wananchi hao na Njalamoto, zilisema baada ya kueleza malalamiko yao kuhusu kasoro nyingi zilizosababisha mgogoro huo na masikitiko kuhusu tangazo la wizara, Njalamoto alimpigia simu Kamishna wa Ardhi, kutaka maelezo ya kina kuhusu tangazo.
Hata hivyo habari zilisema Kamishna huyo katika hali ya kushangazwa, alikana kulitambua tangazo hilo lakini alipobanwa kuwa iweze asilitambua wakati amelisaini yeye, alijibu kuwa labda alilisaini bila kujua kwa kuwa alipelekewa kusaini tu.
Inasemekana kaminisha huyo alitaka suala hilo aulizwe Mkurugenzi wa Mipango miji.
Habari zilisema Mkurugenzi wa Mipanago Miji kwa upande wake, alisema wananchi 29 tu ndio wenye viwanja vyenye matatizo ya msingi na kwamba wananchi wengine ni wakorofi tu wanaopinga mradi wa uendelezaji wa mji wa pembezoni, katika eneo hilo.
Baada ya kikao hicho wasaidizi wa Waziri mkuu, waliondoka kwenda wizarani Ardhi, ili kushughulikia malalamiko hayo na kuwaahidi wananchi hao kuyatafutia ufumbuzi haraka


serikali iko tayari kuilipa kampuni hewa ya dowans maelfu ya mamilioni lakini haiko tayari kuwalipa wananchi wa kwembe vijisenti vyao

JAMANI;;;
 
Wewe hii umeitoa wapi ni ya zamani sana? Uwe unasoma kabla ya kupost
 
Back
Top Bottom