Wananchi wa Kimandolu kuandamana kumng'oa Diwani wa CHADEMA

MJINGA KWA WOTE

New Member
Feb 24, 2016
2
4
Wananchi wa Kata ya Kimandolu wameapa kuandamana mpaka kwa mkurugenzi wa jiji la Arusha tarehe 2/05/16 kushinikiza Diwani wao kuondolewa madarakani.

Hayo yalisemwa jana na wananchi wa mtaa wa Tindigani, Ngaranumbe na Kitiengare wakiwa katika kazi ya kujitolea kurekebisha miundombinu ilioharibiwa na mvua kubwa na mafuriko makubwa sana yaliosababishwa na wachina wanaotengeneza barabara ya Arusha Moshi kuelekeza maji yote kwenye makazi yao.

Mhamasishaji wa maandamano hayo, walioyaita yatakuwa ya amani, ndugu Simion Lengishu, alisikika akisema, pamoja na matatizo ya mafuriko, and miundombinu kuharibika, hawajawahi kumwona diwani wala mbunge toka wamewachagua mwaka jana.

"Tumemwita diwani zaidi ya mara 6 sasa,amekataa kuja kutuona, badala yake ameendelea kuwanyonya wananchi kwa kuwaomba fedha kupitia taasisi yake ya kidini". alisema Julius Koilah wa Tindigani.

Leo alikuwa na habari ya kazi hii, ameahidi kuja, lakini mpaka sasa hivi saa 12 hajaonekana na hajatoa hudhuru.

Wiki tatu zilizopiuta, barabara ya Suye kanisani iliharibika sana, tukamwita tujadili akakataa kuja, ikabidi tukampigie Mayor wa zamani wa Arusha ndugu Lymo magoti akatupatia grader lilokwangua barabara ikawa afadhali.

Mama Grace Shukuru, mwalimu mstaafu wa shule ya kata alisema Lema na Diwani ni majipu maana ahadi walizotoa za kitapeli miaka 6 iliopita hakuna hata moja inafanyika na sasa wametoweka.

Mmoja wa mchungaji wa kanisa la kiroho amesema "hatuwaiti watupe fedha, bali wasaidie hata uhamasishaji, lakini nadhani hii kata tumemkabidhi mhuhuni"

Nilipomtafuta diwani kwa simu yake ya mkononi kujua maoni yake, alijibu kwa kifupi "nipo kwenye kikao cha muhimu halmashauri"

Kwa maoni yetu, ni wakati mwafaka sasa viongozi wa kitaifa wa chadema kutathmini utendaji wa viongozi wao walioshinda kuanzia ngazi ya mtaa, akiwepo bwana Lema mwenyewe.

Nawakilisha
 
arusha nawashangaa sana kuchagua viongozi wakuja kuwaongoza hawana uchungu na wananchi wako kwa ajili ya matumbo yao tu,,wangechagua waarusha wenzao wamgewasaidia
 
Mkuu acheni lawama za kijinga na kuwachafua viongozi wenu mitandaoni. Hizo mnazotumia niakili ndogo sana kurusha makombora kwa diwani na mbunge.

Kawajibuni yupo kwenye kikao halmashauri, huenda alikua akijadili kuhusu suala hilo hilo la kwenu huko. Lema unamrushia mawe bure tu sijui ulitaka wewe ndio uwe mbunge au diwani..

Unaposema Lema hajafanya chochote kwa mwaka wa sita huu unajidanganya na naanza kupata hofu huenda wewe si mkazi wa arusha bali umepita tu. Unafikir Lema angekua zombi kama uwazavyo wana-Arusha wangemrejesha bungeni awamu hii.?

Huenda ulitaka kutoa ripoti yenye ujumbe wa maana kwa viongozi hawa ila umekosea tu namna ya kuuleta hapa.
 
mi nipo arusha hapa lema hajafanya chochote CHADEMA arusha ni mzigo kwa wananchi
 
Aya umesika fanya haraka ukachukue buku 7 zako lumumba
 
Mkuu huku hatuna ubaguzi wa kikabila wala udini. Hapa tunampa hata mkurya chamsingi tu awe na hoja za msingi. Mleta Uzi ana yake ya moyoni au tuseme ana gubu japo pia ID yake inanipa jibu.
arusha nawashangaa sana kuchagua viongozi wakuja kuwaongoza hawana uchungu na wananchi wako kwa ajili ya matumbo yao tu,,wangechagua waarusha wenzao wamgewasaidia
 
arusha nawashangaa sana kuchagua viongozi wakuja kuwaongoza hawana uchungu na wananchi wako kwa ajili ya matumbo yao tu,,wangechagua waarusha wenzao wamgewasaidia
Ni heri kuwa masikini wa kipato kuliko kuwa masikini wa akili kama wewe
 
Mkuu acheni lawama za kijinga na kuwachafua viongozi wenu mitandaoni. Hizo mnazotumia niakili ndogo sana kurusha makombora kwa diwani na mbunge.

Kawajibuni yupo kwenye kikao halmashauri, huenda alikua akijadili kuhusu suala hilo hilo la kwenu huko. Lema unamrushia mawe bure tu sijui ulitaka wewe ndio uwe mbunge au diwani..

Unaposema Lema hajafanya chochote kwa mwaka wa sita huu unajidanganya na naanza kupata hofu huenda wewe si mkazi wa arusha bali umepita tu. Unafikir Lema angekua zombi kama uwazavyo wana-Arusha wangemrejesha bungeni awamu hii.?

Huenda ulitaka kutoa ripoti yenye ujumbe wa maana kwa viongozi hawa ila umekosea tu namna ya kuuleta hapa.
Nakushukuru sana mkuu kwa kuliona hilo,ingawa sipo arusha lkn naamini huyo mleta mada ni mtumwa wa mawazo na siasa za maji taka
 
Back
Top Bottom