Mamia ya wananchi wa Kata za Nyakaliro na Irenza walijitokeza kwa wingiJulai 3, 2025, kushuhudia makala za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Buchosa, chini ya uongozi wa Mbunge wao Eric Shigongo
Zoezi hilo limeendelea kufanyika katika kata hizo ambapo wananchi waliwasilishiwa kazi mbalimbali zilizotekelezwa kupitia video halisi, ikiwemo ujenzi wa shule, barabara, zahanati, huduma za maji safi, chuo cha ufundi, pamoja na mipango ya uwezeshaji kwa vijana na wanawake.
Miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Mbunge huyo na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo katika maeneo ya pembezoni kama Buchosa
Lengo la zoezi hilo ni kufikisha taarifa za maendeleo kwa uwazi, kwa kuwaonesha wananchi hatua zilizofikiwa kwa njia ya video kutoka maeneo husika, hivyo kuimarisha uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi.
Zoezi hilo linaendelea kufanyika katika kata mbalimbali za jimbo hilo, likiwa ni sehemu ya kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kikamilifu katika safari ya maendeleo ya Buchosa
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025