Hiyo pesa badala ya kunufaisha wenye magari ingetumika kuchimba visima kila kijiji na kujenga sekondari za bweni kila kata watoto wasome na kina mama wasisumbukie maji kama ilivyokuwa chini ya ccm. Karata ikichezwa vibaya bila focus itawagharimu cdm. Muda uliobakia kuelekea 2015 ni kidogo sana, mbunge mpya angeanza kusimika alama kila kijiji ili hata ccm wajue hawana chao huko tena. Akitapanya resource ya ukubaliko wake atakumbuka sana baadaye kwa uchungu. Akumbuke historia ya Mrema kusukumwa na umati wa watu kwenye gari lakini na amri ya siku saba mpaka kirarachi walimfuata huko na kuacha kitu kidogo, akasomwa tabia yake mbaya na akaandikiwa umarufuku kuwa rais milele hata haelewi mpaka sasa nini kilitokea. HUO NI USHAURI WA BURE KWA CDM Arumeru mashariki. Kuwa kimya lakini matendo yaseme sana, utaheshimiwa zaidi. mbwembwe zina madhara ya kudumu.