Wananchi vs Viongozi: Nani wazalendo na wapi wasio wazalendo?

Mdomo Mwepesi

Member
Apr 19, 2011
67
93
Tumekuwa tukiambiwa mara kwa mara na viongozi wetu kwamba sisi wananchi tunapaswa kuwa wazalendo kwa nchi yetu huku wakitolea mifano nchi zenye machafuko kama kielelezo cha wananchi kutokuwa wazalendo.

Kati ya viongozi wetu na sisi wananchi nani wazalendo kwa nchi yao? Wananchi tumekuwa wazalendo zaidi na viongozi wetu kutokuwa wazalendo hata kidogo.
Viongozi wetu mngekuwa wazalendo tungekuwa na chenji ya rada?
Viongozi wetu mngekuwa wazalendo tungekuwa na uchafu wa Kagoda, IPTL, mikataba mibovu sekta ya madini na gesi?
Viongozi wetu mngekuwa wazalendo tungekuwa na matumizi mabovu ya fedha ya mifuko ya jamii kwa kujenga majengo yasiyo na tija?
Viongozi wetu mngekuwa wazalendo tungekuwa na ubadhilifu katika taasisi mbalimbali za umma kama unavyoibuliwa na Mkaguzi Mkuu (CAG)?
Viongozi wetu mngekuwa wazalendo kweli tungekuwa na tofauti kubwa ya malipo ya kustaafu kati ya wabunge (miaka) na mfanyakazi aliyefanya kazi zaidi ya miaka 30?

Wananchi tumekuwa wazalendo kupita kiasi lakini viongozi wetu uzalendo wenu kwa nchi una mashaka makubwa, ni wa maneno si vitendo!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom