romaki
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 477
- 218
Chonde chonde watanzania tusikibali kudanganywa, huu mradi tumeujenga sisi na sio hao wadau wa mabasi; sisi ndio tunaodaiwa hela na bank ya dunia na sio hao wadau wa mabasi, sasa iweje tujenge mradi alafu waje watu flani ndo wanufaike wao na familia zao alafu sisi badala ya kunufaika na mradi wetu tunanyonywa zaidi na nauli za bei juu? bei wanazotaka hao wadau ni kubwa sana,
UKWELI ni kwamba huu mradi nauli ilitakiwa iwe ya bei chini zaidi ya tunayolipa sasa hivi kwenye mabasi yetu ya kawaida na hii ni kwa sababu haya mabasi hayatakuwa na foleni wala matuta useme garama zake hasa mafuta zitakuwa juu kuliko haya ya sasa hivi na ndo maana tunaita mradi wa mabasi yaendayo kasi, hao wadau ingekuwa wao ndo wamejenga hiyo barabara kwa pesa zao hapo sawa lakini tumejenga sisi wananchi na nia ni ili kuleta wepesi kwenye maisha yetu ya kipato cha chini na sio kuongeza uzito,
Kama nauli hazitakuwa chini kuliko mabasi yaliyoko sasa hivi ili kuleta maana ya huo mradi na pia wepesi kwa maisha yetu napendekeza tuyakatae hayo mabasi yao hao wadau alafu hizo barabara zitumike special kwa mabasi yaliyopo sasa hivi tena nauli ingeweza kushuka kidogo na maisha yetu yakaenda vizuri tu. Huu mradi ndani yake kuna majipu yashazaliwa natarajia pia serikali yangu sikivu ya magufuli haitatuangusha wananchi.