Wananchi Shinyanga wamtoa jasho Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Shinyanga wamtoa jasho Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiwi, Feb 24, 2012.

 1. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  [h=2]Wananchi wamtoa Pinda jasho[/h]  [​IMG]
  Wananchi wa wilaya ya Meatu mkoani Shinyanga wamewakataa Mkuu wa Wilaya hiyo, Abihudi Saideya, na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Julius Mjengi, mbele ya Waziri Mkuu, Mizego Pinda, kwa madai ya tuhuma mbalimbali zinazokwenda kinyume cha utawala bora.

  Tukio hilo lilitokea juzi wakati Waziri Mkuu alipokuwa akiwahutubia wananchi katika eneo la Mwanhuzi lililoko katika viwanja vya kituo cha mabasi mjini hapa, hali iliyompa wakati mgumu Waziri Mkuu.

  Hali ya kuwakataa viongozi hao iliwekwa wazi mbele ya Waziri Mkuu alipokuwa akijibu baadhi ya hoja na malalamiko ya wananchi hao yaliyotolewa kupitia kwa mbunge wao, Meshack Opolukwa (Chadema).

  Wananchi hao walilalamikia mchakato mzima wa kuwaondoa ndani ya Hifadhi ya Wanayamapori ya Makao (WMA) wanakodaiwa kuvamia kinyume cha sheria.

  Akijibu baadhi ya hoja hizo, Pinda alijikuta akijibiwa kwa sauti na mawoye ya wananchi hao wakisema “ondoka na DC wako huyo hatumtaki, ni mwongo.”

  Walidai kuwa Saideya anaidanganya serikalii na kutoa mfano kuwa alimdaganya hata Waziri wa Tamisemi, George Mkuchika, aliyetumwa kutafuta ukweli wa mambo wilayani hapo kuhusiana na utekelezwaji wa zoezi la serikali la kuwaondoa wananchi wanaodaiwa kuvamia WMA.

  Pinda alilazimika kukatiza hotuba yake mara kadhaa ili kusikia walichokuwa wakikisema wananchi hao na kutumia busara kuwatuliza kwa kuwaambia kuwa amesikia wanachosema.

  Alisema kutokana na hali hiyo, ofisi yake itaunda tume nyingine badala ya taarifa aliyopokea kutoka kwa Waziri Mkuchika kuchuguza mwenendo mzima wa jinsi zoezi hilo lilivyotekelezwa ikiwa ni pamoja na kubaini kama walioondolewa WMA utaratibu ulifuatwa.

  Pia tume hiyo itakuwa na jukumu la kubaini ukweli juu ya tuhuma nzito zilitolewa na wananchi hao kuwa Saideya alinunuliwa gari la kifahari aina ya Toyota VX yenye namba ya usajili T147 ASX kutoka kwa mwekezaji mmoja kupitia kwa mwananchi mmoja (jina tunalo) wa jijini Arusha ili ashinikize kupata eneo la uwekezaji na kuwaondoa wananchi katika eneo hilo.

  Pinda pia alisema tume hiyo itafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na alimwagiza Waziri Ezekiel Maige aliyefuatana naye kushughulikia kwa karibu mgogoro huo na wa mipaka ya hifadhi za Ngorongoro, Serengeti, Maswa Game Reserve na WMA.

  OCD Mjengi ambaye ni mara yake ya pili kukataliwa mbele ya Pinda, wananchi wanamtuhumu kwa uongozi wake wa kibabe na kubambikia watu kesi na unyanyasaji na kwenda kinyume cha dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

  Kwa mara ya kwanza alikataliwa akiwa wilayani Muleba, mkoani Kagera mwaka 2010.

  Waziri Mkuu Pinda alisema hakuna ugumu wowote wa kuchunguza ukweli juu ya tuhuma zinazowabili Saideya na Mjengi, lakini alisema kuwa hawezi kuondoka nao mara moja kwani siyo utaratibu kwani analazimika kupata maelezo ya kutosha kabla ya kuchukua hatua na ikiwa itabainika kuna ukweli atachukua hatua mara moja.

  “Siwezi kuondoka nao leo, kwani siyo utaratibu, ni lazima nipate maelezo ya kutosha kabla ya kuchukua hatua nyingine, kama kuna mapungufu, sisi kama viongozi tutachukua hatua,” alisema na kuongeza:

  “Suluhu ya haya yote ni timu hiyo itakayofanya kazi kwa niaba yangu na Waziri Maige ambaye tunaye hapa atashughulikia.”

  Awali, wakazi wa vijiji saba vilivyopo kandokando ya eneo la hifadhi ya WMA walipinga agizo la serikali linalowataka kuondoka katika maeneo hayo na kutishia kwenda mahakamani.

  Hatua hiyo inafuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga na Saideya likiwataka kuwa wawe wamehama ndani ya siku 30 na kwamba baada ya siku hizo watahamishwa kwa nguvu, hatua iliyotekelezwa kati ya Novemba 10 hadi 15, 2011. Kaya zaidi ya 600 ziliondolewa na kuzua malalamiko.

  Wananchi hao walidai kunyanyaswa na kuchomewa nyumba zao na wengine kujifungulia porini na familia zingine kupoteza watoto wao na kuishi porini huku wakinyeshewa mvua na kukosa chakula.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  ingekua lowasa hapo hapo dc na ocd hawana kazi!pinda haeleweki hana maamuzi...polisi kwa sasa ndiyo kero kubwa
   
 3. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ombwe la uongozi si lazima washuke malaika waje watusemee,tumeshindwa uthubutu kwa maamuzi yenye kukidhi matakwa ya wananchi.Hatuwezi kila siku kuwa kichwa cha mwendawazimu viongozi kujifunzia kunyolea.Sisi ndo wananchi wenye dhamana ya kuwataka wale waliopo kwa manufaa yetu,ikiwa hata dhamana yetu inapuuzwa kuna haja gani ya kuwa na waziri mkuu asiye kunjua makucha yake.Sisi tunasema kitendo cha waziri mkuu kushindwa kutoa maamuzi huo ni uoga uliokithiri na kama yeye hawezi kuwatoa yeye aachie kiti chake wapo Watanzania wengi wenye sifa na uthubutu wa kufanya maamuzi magumu.
   
 4. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  viongozi wachukue maamuzi magumu.
   
 5. B

  BMT JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  nmepoteza iman kwa pinda jaman,kaz ipo
   
 6. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona hajawahi kunyooka. Kabla na baada kuingia madarakani akili yake imepnda tu. Kazi yake kubwa ni kulia lia tu kama mwanamke kahaba. Pinda ni hivyo sana, hafai.
   
Loading...