elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
Wananchi wa Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma wamemshukuru sana Rais John Pombe Magufuli kwa kuwaajengea hospitali ya Kisasa baada ya kutaabika kwa miaka yote wakiwa katika mazingira magumu sana kwa kufuata huduma ya Afya katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga.
Shukran hiyo imepokelewa na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya Kikazi wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayo simamiwa na Ofisi yake.
Katika ziara hiyo Waziri huyo wa TAMISEMI amewapongeza viongozi na wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuhakikisha hospitali hiyo inakamilika vyema.
Aidha, Jafo amewataka wananchi hao watambue kwamba ujenzi wa hospitali hiyo pamoja na vituo vingine virat vya Afya, ujenzi wa miundombinu ya shule, na ujenzi wa barabara ya Lami kutoka Mbinga hadi Bambabay ni upendo wa moyoni wa Dkt. John Pombe Magufuli kwani ameamua kuwatoa katika kisa cha matatizo walichokuwa nacho kwa miaka yote.
Jafo amewaagiza viongozi kusimamia miradi yote iliyoletwa wilayani humo ili miradi hiyo ikamilike kwa lengo la kuwaletea wananchi unafuu wa kupata huduma mbalimbali za kijamii.