Uchaguzi 2020 Wananchi msipige kura za hasira

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,375
3,655
Tunapoelekea siku ya uchaguzi mkuu mwaka 2020, Raia na Wananchi wengi wenye vyama na wasio na vyama wana hasira za kuindoa serikali ya Chama Cha Mapinduzi hali ambayo inaweza kusababisha kura nyingi za CHADEMA kuharibika kwa sababu wapiga kura wengi ni vijana ambao asilimia kubwa ni mara yao ya kwanza kupiga kura

Hivyo vijana wafundishwe namna ya kupiga kura sababu joto la uchaguzi litachangia kuharibika kwa kura nyingi.

Katika karatasi ya kupiga kura, vijana wengi wanapokua wanapiga kura wanakua na mchecheto mpaka wanapiga Vema kubwa ambayo inatoka nje ya kibox hivyo kura inahesabiwa imeharibika.

Tulinde kura zetu vizuri na Magufuli tumrudishe Chato akapumzike.

Tanzania mpya inakuja.

Nawasilisha.
 
Ushauri mzuri sana.

Nawakumbusha tu watanzania.
Tanzania ni moja kati ya The Poorest Countries in the World inashika nafasi ya 8 kutoka chini. ( Focus economy 2019- 23)

CCM imetufikisha hapa
 
Japo kuna muda huwa 'simwelewi' Mwenyekiti wangu Taifa na Mgombea Ubunge wangu nae ana 'Ukakasi' mwingi ila 'Kura' yangu nitaipigia CCM.
 
Aah wapi hatuambiliki this time. Kura zetu tunampa Lissu kwa hasira zote. Manyanyaso yote haya tusiwe na hasira kwa nini?
Rudia kusoma tena hadi mwisho. Mleta mada anachosema, husipige kura kwa hasira hadi ukajikuta unaharibu kura yako. Unaweza kuingia kwenye chumba cha kupiga kura. Ukapewa karatasi ya kura. Unaiangalia hiyo karatasi unaona sura ya Magu akikuangalia na lile tabasamu lake la kinafki. Sasa kwa hasira za kuona sura ya Magu unakwenda kwenye kisanduku cha Tundu Lissu unaweka tiki kuuuuubwa hadi inatokeza nje ya kisanduku. Kwa tiki yako kutokeza nje ya Kisanduku, kura yako inakuwa imeharibika.
 
Watanzania wengi wamechoshwa na ccm Ili Hali maisha yamekuwa magumu kuliko ulaya. Kwa mantiki hiyo watu wengi watapiga kura za hasira Ili kuiondoa ccm madarakani.maisha ya mtanzania yamekuwa magumu use umedoma au la,uwe una kazi au la, uwe mkulima au la,uwe mfanyakazi la,uwe mvuvi au ala, dada powa mjini wanalia, bar zimefungwa hakuna wateja,fedha mtaani shida,biashara shida,ajira shida, ukiuliza unaambiwa SGR,ndege,bwawa la umeme jamani,? Maisha ya watu vipi hakuna mwenye jibu.
 
Back
Top Bottom