Wananchi kususia Wabunge wa Mufindi

Wananchi kususia Wabunge wa Mufindi

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
16,099
Reaction score
24,338
mbunge mufindi kihenzile.jpeg
1111.jpeg

mbunge mufindi kaskazini-mgimwa.jpeg

Mkoa wa Iringa ambao ni Ngome kuu ya CCM na mkoa wenye UFUKARA ULIOPINDUKIA huku ukijikwamua kwenye ukinawara wa UKIMWI, una wabunge wengi lakini jimbo la Mufindi liligawanywa na kuwa na majimbo mawili, moja la kaskazini. na lingine la kusini.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Ndugu, Exaud Kigahe kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Hon. David Mwakiposa Kihenzile mtoto wa 1984 ambaye ni mbunge wa Mufindi kusini hakuna kitu wamefanya Bungeni, kwenye halmashauri wala kwa mafukara wa jimbo hilo huku utajiri ukivunwa na makampuni ya Dar es salaam na wana mufindi wakiwa manamba kwenye mashamba ya chai na miti.
Wabunge hawa wawili bila aibu utashangaa 2025 wanadhubutu kutaka tena fomu za kuomgombea, ikumbukwe waliingia kwenye ule UCHAFUZI WA 2020 wa shujaa!

Zaidi ya malori 25 ambayo yanasafirisha bidhaa mbalimbali kutoka kiwanda cha karatasi Mgololo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa yamekwama kwa zaidi ya siku tano katika Kijiji cha Nyamande na Kitandiliko Halmashauri ya Mji wa Makambako Wilayani Njombe kutokana na ubovu wa barabara katika eneo hilo.Madereva wa magari hayo wamesema changamoto kubwa katika eneo hilo ni Wakala wa barabara kuweka kifusi chenye tope na kusababisha magari kukwama hasa katika kipindi hiki ambacho mvua inanyesha na kuiomba Serikali kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami au changarawe kwani imekuwa na mchango mkubwa kiuchumi.
Inasemekana kundi la CHAWA wameandaa PUNDA kwaajili ya kumpokea "mtoto pekee"huko Arusha!
 
Aiseh!!

Mimi kama mwenyekiti wa CCM nawafuta uanachama kabisa kama hawana juhudi za dhati kutatua changamoto za wananchi!

Wanakihujumu chama!!
 
Wilaya ya Mufindi ni tajiri sana kama ilivyo kwa Wilaya za Kilombero, Mlimba, Ulanga na Malinyi! Na imekuwa ikiingizia serikali pesa nyingi kutokana na uwepo wa viwanda mbalimbali na pia mazao ya biashara kama miti ya mbao na chai!

Ila katika hali ya kushangaza, barabara zake ni za tope! Na kipindi cha mvua zimekuwa zinapitika kwa shida sana! Sasa mtu mwenye akili timamu atajiuliza hivi yale mapato yatokanayo na ushuru/kodi mbalimbali; huwa yanapelekwa wapi?

Ni kwa nini hii serikali haitoi kipaumbele kujenga barabara za lami kwenye hii Wilaya ya Mufindi ili kurahisisha usafirishaji hayo mazao ya biashara na pia hizo bidhaa za kutoka kiwanda cha karatasi Mgololo?

Kinachouma hii Wilaya haijawahi kupata Wabunge wenye kupigania uboreshaji wa miundombinu ya barabara! Wao mara nyingi wakiwa bungeni utawakuta wanawekeza nguvu kubwa kwenye kuitetea serikali ili wateuliwe kuwa Mawaziri!
 
View attachment 2953650View attachment 2953653

View attachment 2953652

Mkoa wa Iringa ambao ni Ngome kuu ya CCM na mkoa wenye UFUKARA ULIOPINDUKIA huku ukijikwamua kwenye ukinawara wa UKIMWI, una wabunge wengi lakini jimbo la Mufindi liligawanywa na kuwa na majimbo mawili, moja la kaskazini. na lingine la kusini.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Ndugu, Exaud Kigahe kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Hon. David Mwakiposa Kihenzile mtoto wa 1984 ambaye ni mbunge wa Mufindi kusini hakuna kitu wamefanya Bungeni, kwenye halmashauri wala kwa mafukara wa jimbo hilo huku utajiri ukivunwa na makampuni ya Dar es salaam na wana mufindi wakiwa manamba kwenye mashamba ya chai na miti.
Wabunge hawa wawili bila aibu utashangaa 2025 wanadhubutu kutaka tena fomu za kuomgombea, ikumbukwe waliingia kwenye ule UCHAFUZI WA 2020 wa shujaa!

Zaidi ya malori 25 ambayo yanasafirisha bidhaa mbalimbali kutoka kiwanda cha karatasi Mgololo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa yamekwama kwa zaidi ya siku tano katika Kijiji cha Nyamande na Kitandiliko Halmashauri ya Mji wa Makambako Wilayani Njombe kutokana na ubovu wa barabara katika eneo hilo.Madereva wa magari hayo wamesema changamoto kubwa katika eneo hilo ni Wakala wa barabara kuweka kifusi chenye tope na kusababisha magari kukwama hasa katika kipindi hiki ambacho mvua inanyesha na kuiomba Serikali kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami au changarawe kwani imekuwa na mchango mkubwa kiuchumi.
Inasemekana kundi la CHAWA wameandaa PUNDA kwaajili ya kumpokea "mtoto pekee"huko Arusha!
Heka heka za mapokezi zinaandaliwa. Mbunge wetu mpendwa tunategemea atoe neno la kukaribisha mkombozi wa wanyonge
 
Back
Top Bottom