Wananchi hawajafungika kutoa mawazo yao - UVCCM

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
6.jpg


Na Khadija Khamis,MAELEZO Zanzibar


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi umesema wananchi hawajafungika kutoa mawazo yao katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba,lakini msimamo wa CCM ni kubaki katika mfumo wa muundo wa Serikali mbili.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mjini hapa Jana, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzíbar, Jamal Kassim Ali alisema kimsingi wananchi wako huru kutoa maoni yao kuhusu aina ya mfumo wa Muungano,lakini kwa wanachama wa CCM ni lazima wafuate msimamo wa Chama hicho.



Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kwamba Umoja wake unaamini katika kulinda na kuhifadhi umoja na mshikamano uliopo hivyo ni muhimu kwa wananchi kutokubali kushawishiwa kuvunja Muungano. “Katika suala la Muungano, CCM imeweka wazi kuwa itaendeleza muundo wa Muungano wa Serikali mbili kama inavyoelezwa katika ibara ya 221(a) ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi sisi hatuwezi kuikiuka katiba hiyo” Alisema Jamal.


Naibu Katibu Mkuu huyo alisema Vijana wa CCM wanakubaliana na muongozo wa Chama hicho hasa katika suala la Muungano wa Serikali mbili ikiwa miongoni mwa mambo 15 ya msingi yaliyopendekezwa na Chama hicho kuwa yawemo katika katiba mpya.


“Tunakubaliana na suala la kuyatoa katika orodha ya mambo ya Muungano yale yote yanayoikwaza Zanzíbar kiuchumi ikiwemo suala la mafuta na gesi asilia, ushuru wa forodha, mikopo ya nje” Alisema Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzíbar.


Jamal alisema kuwa vijana wa CCM wanaamini kasoro zilizokuwepo katika Muungano zinazungumzika na kurekebishika kwa hivyo hakuna haja wala sababu ya watu kufanya fujo au kutumia matamshi ya jazba lililo muhimu ni wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Jaji Warioba ambayo tayari imeanza kazi ya kuchukua maoni.


Wakati huo huo, Baraza la Wazee CCM kupitia Baraza lao la ushauri wamesikitikishwa na baadhi ya vijana kufanya vitendo vya kuashiria kuvunja amani na umoja wa nchi. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Makame Mzee Suleiman, alisema wamechukizwa kuona baadhi ya viongozi akiwemo Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakitumia picha yake wakati akihutubia wanachama wa CCM kwa madhumuni yasiyokuwa yake.


“Lakini kama yote hayo hayatoshi kutukera sisi wazee tunalaani kwa kauli moja walioeneza vipeperushi kumuhusisha Rais wetu mpendwa Dk. Ali Mohammed Shein juu ya suala zima la kuridhia Muungano wa mkataba” Alisema Mwenyekiti Makame Mzee.


Katika taarifa hiyo Baraza la Wazee walisema kwamba katika vipeperushi hivyo anaonekana Rais Dk Shein akiwaelezea mamia ya wana CCM jambo hilo halikuwa la kweli na wamewataka wanaharakati waseme yao wasiwasemee viongozi wala wnanchi.


Baraza hilo limeshauri wananchi waachwe kuingia kwenye mchakato wa katiba watoe maoni yao juu ya katiba ili hatimaye Tanzania ifikie katika lengo lililokusudiwa la kupata katiba mpya


Imewekwa na MAPARA at 7:22 PM
 
sasa nini maana ya kutaka watu watoe maoni huru wakati tayari ccm mna msimamo wenu na mmejiapiza kuwa kamwe hautabadilika!
 
Katiba mpya haiwezi kupatikana chini ya usimamizi wa kibazazi wa CCM. Katiba mpya ianze na kuiondoa CCM. Vinginevyo tunafungana kamba. Asiyeamini hili atanikumbuka siku moja kuwa Father of All yaani baba yenu nyote alisema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom