Wananchi Baneni Wabunge kwa Masilahi ya Taifa na sio ya Jimboni

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,507
Wabunge trick wanazo tumia ni kupitisha kila kitu pale Dodoma wakijua kabisa hakihusiani na Jimbo, na walisha jua Jimboni wananchi wanataka Tangible na sio Policy.

Ndio maana huwezi ona mbunge ana adhibiwa na wapiga kura wake kisa kaunga mkono sheria kandamizi pale Dodoma.

Wananchi wana angalia ni Mbunge kapeleka Bati, Cement, Misumari, kachangia pesa basi. Hivyo ndio vitu wanavyo angalia.

Usha muona mbunge kama Abood anao ngea chochote pale Dodoma? Ila vipo jimboni kwake na Magari ya kubebea maiti?

Hawa wakina Msukumu wanacheza na akili za wajinga, Huyo Msukuma anapitisha kila kitu pale Dodoma then anajifanya ni mtoa ushauri mzuri sana.

Na wabunge walisha jua fika raia hawana time na Mambo ya kitaifa.

Nikuulize hivi wana nchi wa Kibondo Kigoma ukiwaambia Bandari imeuzwa wanakuelewa kitu? Ukiwambia Wamasai wa ngorongoro kwamba Mbunge wao kaunga mkono uuzwaji wa Bandari watakuelewa? Wewe waambie kaunga mkono kuuzwa Ngorongoro hapo watakuelewa.

Pale Dodoma ndio kuna tatizo Wabunge wakisha pitisha madudu hukimbilia Jimboni na Mabati au Cement kwenda kuwahadaa raia wao.
 
Back
Top Bottom