Wananchi achaneni na huu upuuzi mara moja!

Wananchi achaneni na huu upuuzi mara moja!

Echisute

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2018
Posts
635
Reaction score
633
Leo tar. 09.07.2026 majira ya saa 3 asubuhi, kata ya Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora kuna tangazo limetangazwa likawataka wakazi wote pamoja na vitongoji vyake kesho asubuhi majira ya saa 4 waache shughuli zao zote waende kumlaki Ridhiwan Kikwete eti kwa sababu atakuwa anazindua shule mpya ya secondary hapo katani.

Tangazo limeenda mbali na kusisitiza marufuku ya mtu yeyote kuonekana akirandaranda bila kuwa eneo la tukio au kufunguliwa kwa aina yoyote ya biashara kabla ya huo ugeni kuondoka hapo katani! Onyo limetolewa kwa mfanyabiashara yeyote atakayekiuka masharti ya hilo tangazo kutozwa faini ya Tsh. 50,000/=

My take: Naomba chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) mtoe elimu kwa wananchi wote nchi nzima mkilaani na kukemea matamshi ya vitisho kama haya na kuwajengea wananchi uelewa wa kutambua haki zao za kufanya shughuli zao za kiuchumi bila kuathiriwa na matamshi ya kisiasa kama haya.
 
Unategemea nn kuongozwa na ccm?akili mgando tangia miaka ya 70 hadi leo.wameshndwa kubadilika na nyakati
 
Unategemea nn kuongozwa na ccm?akili mgando tangia miaka ya 70 hadi leo.wameshndwa kubadilika na nyakati
Shame on them. Yaani kesho wananchi wote wamezuiwa kufanya shughuli zao halali za kuwaingizia kipato eti kwa sababu ya mpumbavu mmoja anaitwa Rizmoko. Ccm ni wapumbavu sana mkuu!
 
Tangazo ni la maneno tu au ni la maandishi, kama ni la maandishi ungelipiga picha na kulitupia humu ingekuwa poa sana
 
Tunarudi enzi ya nyerere mnamsubiri barabani kuanzia asubuh hadi jion hakuna kula.bwana mkubwa anapita
 
Tangazo ni la maneno tu au ni la maandishi, kama ni la maandishi ungelipiga picha na kulitupia humu ingekuwa poa sana

Tangazo ni la maneno tu au ni la maandishi, kama ni la maandishi ungelipiga picha na kulitupia humu ingekuwa poa sana
Wametangaza kwa kutumia speaker kama zile zinazotumika mostly misikitini mkuu. Ikitokea baadae nikaliona la maandashi nitalitupia humu bila shaka yoyote!
 
Back
Top Bottom