Wanakijiji wavamia eneo la Kanisa wampiga Padre Handeni Tanga.

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481

Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani handeni imelazimika kutumia nguvu kuwaondoa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kwamkono kilichopo kata ya Sindeni waliovamia na kujimegea maeneo ya ardhi kwa nguvu zaidi ya hekta 5 zinalomilikiwa na Kanisa Aglikana Dayosisi ya Tanga kisha kujenga nyumba za kuishi na kulima mazao ya chakula.

Sakata hilo linafuatia mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo kuwaendea wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Handeni chini ya mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya hiyo Husna Msangi na kuwatolea lugha za vitisho kisha kuwaamuru waondoke shambani hapo hatua iliyosababisha viongozi wa kamati hiyo kuingilia kati baada ya kuelezwa kuwa hata padre wa kanisa hilo ni miongoni mwa waliopata kipigo kutoka kwa wananchi.
Awali Katibu wa Mipango na Maendeleo Kanisa Anglikana la Mtakatifu Francis lililopo Kwamkono wilayani Handeni Bwana Daud Mpalahingwe amelalamikia viongozi wa Serikali ya kijiji hicho kwa kuuza kwa makusudi eneo la kanisa kwa kuidhinisha makubaliano baina ya wanakijiji na wageni wanaohitaji kujenga na kulima bila maafikiano na wamiliki wa maeneo hayo.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa wilaya alilazimika kuwaamuru wakazi waliojenga na kulima eneo la kanisa kubomoa mara moja nyumba zao kabla nguvu za kisheria hazijatumika.

Chanzo: ITV
 
Yani wana nchi wa serikali ya magufuli wao hawajui sheria , hata kidogo wao hawautukituiitwacho...utaratibu wana ncnchia Tanzania ya mamaguiniAHAPATWENDEUTUShagalabagala wana nchi wa magu wao wakiona mtu mwenye mali zaidi yao kwao wao niyakwao...kila shamba wao nila kuchukua tu.
 
Tatizo Magufuli sometimes na yeye hafuati sheria ndo wananchi na wao wanaona wako juu ya sheria
 
Yani wana nchi wa serikali ya magufuli wao hawajui sheria , hata kidogo wao hawautukituiitwacho...utaratibu wana ncnchia Tanzania ya mamaguiniAHAPATWENDEUTUShagalabagala wana nchi wa magu wao wakiona mtu mwenye mali zaidi yao kwao wao niyakwao...kila shamba wao nila kuchukua tu.
Pole Mkuu, naona umeandika ukiwa na hasira sana, hii Ndiyo trend tunayoitaka wananchi siyo kuoneana.
 
Yani wana nchi wa serikali ya magufuli wao hawajui sheria , hata kidogo wao hawautukituiitwacho...utaratibu wana ncnchia Tanzania ya mamaguiniAHAPATWENDEUTUShagalabagala wana nchi wa magu wao wakiona mtu mwenye mali zaidi yao kwao wao niyakwao...kila shamba wao nila kuchukua tu.
Huo sasa ni uongo. Wananchi kujichukulia sharia mikononi imeanza lini. Nami kuna thread nyingi tu nilikuwa naandika kupinga hili tendo la kujichukulia sharia mikononi! Lakini kuna baadha walikuwa wanaliunga mkono sasa tunaelekea pabaya namuomba mh. JPJM akemee hili kwa kuwa wananchi wanamsiku=iliza na atakaikiuka achukuliwe hatua kali na hii iwe kwa wote hata watuhumiwa wa Wizu=I sharia ndio ifuatwe and not other wise!
 
Back
Top Bottom