maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,296
- 15,559
Wakuu kesho ndio ile siku ya kwenda ku-enjoy na kuburudika na kubadili mazingira mjini Moshi kwenye KiliMarathon. Binafsi hii itakua mara yangu ya kwanza kushiriki na hapa nimeshapack kila kitu tayari kwa safari mida ya mchana hivi. Nafurahi kwa sababu nakutana na wadau wengine kutoka pande mbalimbali za TZ ambao tutakutana jioni ya leo mjini Moshi. Nimepanga kukimbia mbio za Km 5 na nimeshalipa Tsh 4,000/. Kama nawewe ni miongoni mwa watakaoshiriki tukutane hapa tupeane mawazo na kama ulishawahi kushiriki tupia mauzoefu yako huwa inakuaje na nini kilikuvutia ama kukufurahisha zaidi.