WanaJF nisaidieni kibarua nivuke hii transition period

Kanjunju Leo

Member
Apr 6, 2021
7
3
Wakuu heshima kwenu,

Nakuja kwenu nikiwaomba kwa yeyote anayeweza kunisaidia nipate kibarua ili walau niweze kupata fedha ya kula anisaidie..Niko tayari kufanya kazi ngumu ya kutumia nguvu(saidia fundi,store za nafaka n.k) au kusimamia chochote au kazi nyingine yoyote

Umri miaka 24.

Elimu:University lakini sijafanikiwa kumaliza

Nipo Dar es Salaam.
 
Kama unatokea sem-village tafuta eneo wapigishe tuit watoto
 
Mimi pia natafuta msaada wenu

Naitwa kassim

Naishi dsm mbagala

Yoyote hata kuuza chips na zingine zisizo na elimu

0714945058
 
Nashauri JF waanzishe Uzi wa kusaidia vijana wanaotafuta ajira ndogondogo waeleze wanatafuta kazi gani.

Tufahamu kwamba, kuna watu pia wanatafuta vijana wakuwaajiri kwenye shughuli zao ndogondogo kama vile shamba, udereva, nyumbani, dukani n.k.
cc Maxence Melo
 
Kwa sasa kumetokea wimbi kubwa la vijana wanaotafuta kazi kwa ajili ya kujikimu kwenye maisha yao. Hii huenda imesababishwa na Sera zetu mbovu katika masuala ya uchumi, elimu na ajira. Utakuta kijana ni graduates anatafuta kazi hata ya kuuza duka au kuuza chips. Kwa maana hata kama una kiosiki chako huwezi kumwajiri kijana ambaye mmekutana hapa Jf siku moja akuendeshee biashara yako. Hii ni kwa sababu hujui tabia yake mpaka hapo alipofikia. Watu wengi tunaumia sana tukisikia shuhuda za vijana humu Jf namna wanavyosumbuka mara baada ya kuhitimu masomo yao. Ingawa sasa, hata kama tunazo fursa za kuwaaajiri inakuwa shida kuwasaidia. Kwa kweli inabidi Serikali iandae Sera zenye manufaa za kumfanya mhitimu ajiajiri kuliko kutafuta kazi ya kuajiriwa.
 
Wahusika wameziba masikio. Kuna mikopo ile ya halmashauri ambayo hutolewa kwa vikundi vya vijana na wakina mama.

Ila urasimu kila kukicha unaongezeka. Japokuwa hiyo mikopo ingekuwa fursa nzuri ya mitaji kwa vijana angalau kupata kwa kuanzia.

Nilishawahi kushauri waunde timu zinazopita vyuoni kwa wanafunzi wanaomaliza masomo na kusikiliza mawazo yao ya biashara na kuwakopesha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom