yaser
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 1,361
- 299
Yakiwa yamebaki masaa tu kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini mwetu, wananchi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara wameanza kuingiwa hofu na wengine wakiamua kuyakimbia makazi yao na kuhamia nchi ya jirani ya Msumbiji baada ya wanajeshi na magari yao ya kijeshi kutanda katika wilaya hiyo.
Hili suala limeibua maswali na woga mwingi sana miongoni mwa wananchi wa wilaya hiyo wengine wakihoji mbona chaguzi kadhaa zimepita haijawahi kutokea hali hiyo? Alipoulizwa mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendegu amesema wapo pale kuimarisha amani.
Kwa upande mwingne mbunge anayegombea jimbo hilo amesema amepewa rushwa ya shiling milion 160 ila amekataa na sasa anapata vitisho kila muda.
Chanzo: Azam Two (Habari).