Wanajeshi wana ubia gani CCM?

Wanajeshi wana ubia gani CCM?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,512
Reaction score
40,197
Hakuna shaka yeyote kwamba ndani ya CCM kumejaa makada wengi ambao background zao ni wanajeshi ama wastaafu wa jeshi. Ninaposema jeshi namaanisha kada zote za jeshi yaani JWTZ, Polisi, Magereza, Intelejensia na wengineo.

Haiyumkiniki kwamba weledi wa majeshi yetu umeshuka na sasa kutumika kama mbeleko ya CCM kwa sababu ya mwenendo wa chama hicho kuwapatia nafasi za kumega keki ya taifa pale wanausalama hao wanapokuwa wamestaafu am hata wakiwa kazini. Ikumbukwe kwamba mkataba wa kazi baina ya mwajiri na wanausalama wetu ni SIRI kubwa, hivyo kupitia makamanda waliopo jeshini hasa kwenye makambi ya mafunzo wamekuwa wakiwafundisha ama kuwaharibu akili wanausalama wetu ili wawe vyombo vya kuisaidia CCM na si kutekeleza majukumu yao ya kikatiba. CCM ambayo inaamini kuwa itatawala milele inatumia mwanya wa usiri wa mikataba ya ajira ya wanausalama hawa kuweza kujinufaisha kwa kuwatumia maaskari wetu kukitumikia chama na si Nchi kama katiba inavyoelekeza.

Tamko la kamanda Shimbo (Rtd) kipindi kifupi kabla ya ushaguzi mkuu 2010 halikuja kama ajali, bali ilionekana dhahiri kwamba CCM ilielemewa na kulikuwa na uwezekano mkubwa nchi kwenda upinzani hivyo wakielewa kinachoendelea waliamua kutoa angalizo (VITISHO) kuwaasa wapinzani wakubali matokeo. Na hata wakati wa ukusanyaji wa matokeo ya kura kulikuwepo na uthibitisho wa magari ya jeshi kuhusika kukusanya ama kusambaza masanduku ya kura, Pia kuna polisi walikamatwa wakiwa na kura feki ambapo hakuna taarifa za maana kuhusu hatua zilizochukuliwa.

Mifano ipo mingi ya wanausalama ambao hata wakiwa kazini au baada tu ya kustaafu wametimkia siasa na hasa CCM.

2015 kuna uwezekano mkubwa wa yaliyotokea 2010 kujirudia.
 
Wanajeshi ni WAZALENDO namba moja nchini. Wamekula kiapo cha kufa kwa ajili ya kuilinda nchi...
 
Wanajeshi ni WAZALENDO namba moja nchini. Wamekula kiapo cha kufa kwa ajili ya kuilinda nchi...
Hebu tuwekee hapa mkataba wao wa ajira.

Je UZALENDO huo ndo unaowasukuma kuwatwanga risasi raia wasio na silaha?
Ni wazi kwamba operesheni nyingi za polisi dhidi ya raia huwa zinawachanganya na wanajeshi ktk magwanda ya polisi. Hii ni hatari kwa usalama wa nchi.

Katiba inatoa uhuru kwa raia ambao CCM inatumia dola kuuminya uhuru huo
 
Hebu tuwekee hapa mkataba wao wa ajira.

Je UZALENDO huo ndo unaowasukuma kuwatwanga risasi raia wasio na silaha?
Ni wazi kwamba operesheni nyingi za polisi dhidi ya raia huwa zinawachanganya na wanajeshi ktk magwanda ya polisi. Hii ni hatari kwa usalama wa nchi.

Katiba inatoa uhuru kwa raia ambao CCM inatumia dola kuuminya uhuru huo


Mkuu allegations nzito sana hizo. Una ushahidi?
 
Mkuu allegations nzito sana hizo. Una ushahidi?
Unaishi dunia ipi mkuu?
Umesahau ya Mwangosi?
Umesahau ya Zanzibar Jan 27?

Mkuu hizo ni allegations yes na ikiundwa tume huru kuchunguza tutagundua mengi zaidi ya hayo.

Haiwezekani serikali ikatumia nguvu kubwa kudhibiti watu wake huku ikiachia rasilimali zake na uchumi kuyumbishwa na wachache ambao wanatoroshea nje. Ndo maana mashaka makubwa hayapungui juu ya mwenendo wa wanasiasa wetu kulazimisha dola kuwabeba badala ya kuwaacha huru wakitekeleza majukumu yao ya kikatiba
 
Back
Top Bottom