Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuondoka Congo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuondoka Congo

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Apr 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Baraza la usalama la umoja wa mataifa, linatarajiwa kutuma ujumbe katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo siku ya jumamosi, kujadili muda mwafaka wa kuondolewa kwa wanajeshi elfu ishirini wa kimataifa nchini humo.
  Hiki ndio kikosi kikubwa zaidi cha wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani.
  Rais wa nchi hiyo,Joseph Kabila, amesema anataka wanajeshi wote hao kuodnoka ifikapo katikati ya mwaka ujao.
  Ingawa katibu mkuu wa umoja wa mataifa , Ban Ki Moon amependendekea waondoke kwa awamu katika kipindi cha miaka mitatu, ikiwa ni sehemu ya mpango wake kurejesha amani katika nchi hiyo ambapo raia wangali wanashambuliwa na makundi ya waasi.
  Baraza la usalama lina hadi mwishoni mwa mwezi ujao kufanya uamuzi ni lini jukumu lake la kulinda amani litatizamwa upya.  http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2010/04/100414_un_congo.shtml
   
Loading...