Wanajeshi wa Marekani CIA wauwawa na china

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,916
Gazeti la New York Times limeripoti kuwa China, imewauwa au kuwafunga jela majasusi kati ya 18 au 20 hivi wa CIA, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kulemaza kabisa shughuli za Marekani za kuichunguza China.

Afisa mmoja mkuu wa Marekani ameliambia gazeti hilo kuwa, hiyo ni mojawepo ya ukiukaji mkubwa wa usalama, kwa miongo kadhaa na kufananishwa na usaliti wa kutoa siri kwa Urusi na Aldrich Ames (wa CIA) na Robert Hanssen (wa FBI).

Baadhi ya watu sasa wanadhani kuwa China, ilidukua mfumo wa mawasiliano wa CIA, ambayo hutumiwa katika mazungumzo ya kisiri.

Lakini kunao wengine wanaoamini kuwa, mdukuzi alisambaratisha kizuizi cha siri cha wapelelezi wa Marekani, mnamo mwaka 2010.

Majasusi hao walianza kutoweka mmoja baada ya mwingine, kuanzia mwanzo wa 2011 (huku mmoja wao akipigwa risasi mbele ya wenzake katika eneo la kubarizi, kwenye jumba la serikali).

Idara ya ujasusi CIA, imekataa kuzungumzia swala hilo.
 
Nahisi ni yule aliyekuwa anatoa siri za marekani kwa wachina ambae alikuwa ameajiriwa na FBI,japo jina nimemsahau but ni mchina kwa asili na ila kazaliwa USA.Soo now ni wakati wa kazi bin kazi; Nooo kurudi nyuma
 
Cha msingi hpo USA wamkamate huyo aliyetoa siri kwa wachina na kusababisha kuuawa kwa hao maajenti wa CIA anyongweeee kidogokidogo kama mwezi hiv mpk akome na iwe fubdisho kwa wengine.
 
Halafu ndiyo mnasema... Mnataka kutuma maagent wa CIA mkamuue Kim? Mnaonesha ni jinsi gani vyombo vyenu vya usalama vilivyo vya hovyo..... Tukiwadaka N.korea tunawalipuwa na nuke
 
Hao wamedakwa baada ya mmoja kutoa siri,unadhan walidakwa km vifaranga.

Wakt hyo nuke yenu ipo njian wenzenu watakua washawageuza jivu mtabaki historia tu kama mlishawahi kuwepo duniani.
 
Sawa wamekufa kazini ndio uanaume na ujasusi ulivyo halafu ha9 nadhani wengi wao walikuwa ni Double Agent
 
Halafu ndiyo mnasema... Mnataka kutuma maagent wa CIA mkamuue Kim? Mnaonesha ni jinsi gani vyombo vyenu vya usalama vilivyo vya hovyo..... Tukiwadaka N.korea tunawalipuwa na nuke

Mkuu hizo ni ndoto za mchana - wamewai kufankisha operation gani ya maana tangu kuanzishwa kwake - hata ya Pakistan walipo mpiga risasi kwa yule wanaye dai ni Osama walisaidiwa na Jeshi/majasusi wa Pakistan - miaka karibu kumi walikuwa hawajui anaishi wapi, tukija kwa marehemu Mullar Omari alikufa a natural Death CIA wala walikuwa hawajui kajichimbia wapi! Haya tuje kwa Dr. Ayman Mohammed Rabie al-Zawahiri ambaye ndiye Kiongozi wa sasa wa kundi la Al-Qaeda mbona huu ni mwaka karibu wa ishirini CIA wanamtafuta kwa udi na uvumba bila mafanikio - sifa za CIA nyingi ni za kutunga tu kwenye simulizi za former CIA Agents maelezo yao uweka chumvi ili wauze vitabu wanavyo tunga.

Binafsi nachukulia taasisi hii is more like a paper Tiger kuliko kitu kingine - hawawezi kuingia kwenye Taifa mahili kwa ulizi/jasusi wakatoka salama watashikwa kama kuku na kuuwawa inapo bidi, walijaribu kumuua Fidel Castro zaidi ya mara hamsini wakashindwa, kinara aliye kuwa anashinikiza Castro auwawe akauwawa yeye kwa kupigwa risasi(John F. Kennedy), CIA wataendelea kutishia tishia/vuruga Mataifa madogo na siyo yanayo jitambua na kuwa na uwezo kijeshi na kijasusi.
 
Waliouawa au kopotea ni informer wa CIA siyo wanajeshi wao. Mara nyingi informer ni wachina wenyewe na China imekuwa ikilipa watu wake kuwagundua na kuwataja Snitch wa CIA. Hii inatokea dunia nzima siyo uchina peke yake ila nchi nyingine huwa wanawakamata na wanafanya kubadilishana na wafungwa wao. Mchina wale ni watu wao masnitch ndo maana wanawaua na kuwapoteza.
 
Cha msingi hpo USA wamkamate huyo aliyetoa siri kwa wachina na kusababisha kuuawa kwa hao maajenti wa CIA anyongweeee kidogokidogo kama mwezi hiv mpk akome na iwe fubdisho kwa wengine.
Alixhakamatwa kitambo na alikiri kosa lake,sasa cjui wanasubir nn,au wanataka kuona jinsi walivyodukuliwa kizembe ndo waanze kazy
 
Mkuu hizo ni ndoto za mchana - wamewai kufankisha operation gani ya maana tangu kuanzishwa kwake - hata ya Pakistan walipo mpiga risasi kwa yule wanaye dai ni Osama walisaidiwa na Jeshi/majasusi wa Pakistan - miaka karibu kumi walikuwa hawajui anaishi wapi, tukija kwa marehemu Mullar Omari alikufa a natural Death CIA wala walikuwa hawajui kajichimbia wapi! Haya tuje kwa Dr. Ayman Mohammed Rabie al-Zawahiri ambaye ndiye Kiongozi wa sasa wa kundi la Al-Qaeda mbona huu ni mwaka karibu wa ishirini CIA wanamtafuta kwa udi na uvumba bila mafanikio - sifa za CIA nyingi ni za kutunga tu kwenye simulizi za former CIA Agents maelezo yao uweka chumvi ili wauze vitabu wanavyo tunga.

Binafsi nachukulia taasisi hii is more like a paper Tiger kuliko kitu kingine - hawawezi kuingia kwenye Taifa mahili kwa ulizi/jasusi wakatoka salama watashikwa kama kuku na kuuwawa inapo bidi, walijaribu kumuua Fidel Castro zaidi ya mara hamsini wakashindwa, kinara aliye kuwa anashinikiza Castro auwawe akauwawa yeye kwa kupigwa risasi(John F. Kennedy), CIA wataendelea kutishia tishia/vuruga Mataifa madogo na siyo yanayo jitambua na kuwa na uwezo kijeshi na kijasusi.
Unajitahidi utadhna hata USA ushafika
 
Back
Top Bottom