Wanajeshi wa DRC wakamatwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi wa DRC wakamatwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buswelu, Nov 7, 2011.

 1. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jeshi la Tanzania limesema limewakamata wanajeshi 20 waliokuwa wamejihami vikali kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

  Msemaji wa jeshi la Tanzania katika mji wa Magharibi wa Kigoma, amesema wanajeshi hao wa Congo waliingia nchini humo kinyume cha sheria, wakitumia boti, baada ya kuwafukuza wapiganaji wa waasi katika ziwa Tanganyika.


  Ripoti zinasema kuwa wapiganaji hao walikuwa wamejihami na bunduki za rashasha, maguruneti yanayorushwa kwa kutumia roketi na kiasi kikubwa cha risasi.
  Idadi kubwa ya wapiganaji wa waasi kutoka Congo, waliwasili mjini Kigoma siku ya Alhamisi, kutafuta matibabu. Wengi wao walikuwa na majeraha mabaya ya risasi.

  Source :
  http://www.bbc.co.uk/swahili/mobile/habari/2011/11/111107_tanzania.shtml
   
 2. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Duu hatari sana
   
Loading...