Wanajeshi saba Watanzania wauawa Dafur

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
jk.jpg


Dar es Salaam. Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongonimwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katikajimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, miiliyao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.
Hii ni mara ya kwanza kuripotiwakwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.
Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.
Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.
Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081wa kulinda amani katika jimbo laDarfur.
Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.
Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasiwa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.
Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850.
Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi, alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa majeshi ya Tanzania yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia waliuawa wanajeshi wa Tanzania 11.
Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa, alisema.

Source: MCL
===
Updates:
Taarifa - JWTZ wamethibitisha kuwa askari 7 wamekufa na 14 kujeruhiwa huko Darfur...
Kwa sasa mipango ya kuwajulisha ndugu inafanyika, na maandalizi ya Mazishi.
 
jk.jpg


Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
Hapa ndipo napowakubali Wanajeshi, "ameskia lakini si taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi. Angelikuwa yule dada yetu sensa angelisema "ndio kwanza naskia na wewe" na kukata cim. Nadhani wanajeshi wanatumia taaluma na akili zao huwa haziondoki tofauti na polisi
 
Hapa ndipo napowakubali Wanajeshi, "ameskia lakini si taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi. Angelikuwa yule dada yetu sensa angelisema "ndio kwanza naskia na wewe" na kukata cim. Nadhani wanajeshi wanatumia taaluma na akili zao huwa haziondoki tofauti na polisi
Mmmh!! hilo unalolizungumzia lilikua ni lile Jwtz la kipindi cha Nyerere, lakini sio hili la siku hizi linalotekelza amri ya pinda ya kupiga kubaka na kutesa Wanamtwara hovyo,limeshapoteza maana ya kuitwa jeshi la wananchi sasaivi ni jeshi la ccm na la kulinda mafisadi.
 
watu wa mtwara mmepata mahali kutolea uchungu, usishangae 4 kati ya 7 ni wa mtwara..
 
Mbona huwa wanauliwa sana tu, kama kuku, sema wanaficha ficha....
 
Mmmh!! hilo unalolizungumzia lilikua ni lile Jwtz la kipindi cha Nyerere, lakini sio hili la siku hizi linalotekelza amri ya pinda ya kupiga kubaka na kutesa Wanamtwara hovyo,limeshapoteza maana ya kuitwa jeshi la wananchi sasaivi ni jeshi la ccm na la kulinda mafisadi.

Wivu tuu probably! huwezi kushawishi kwa hoja isiyo na mashiko kiasi hicho! wakati wote ni kuhakikisha amani ipo! ukicheza na amani utaumia> wachache walete fujo waachwe hadi ifikie vp? Goverment is the coerssive instrument! hawawezi kufanya kazi kama waseminary hao! unataka wakupigie magoti eti uache fujo?
 
Wewe ni --------,na hukufaa kuwepo humu jamii forums kama home of great thinkers,unashabikia siasa kama ushabiki wa mpira wa simba na yanga.Haihitaji uende shule ili ufahamu kuwa pamoja na matatizo yetu,lakini tunaposhambuliwa na adui wa nje tunapaswa kuwa wamoja na kutetea kwa nguvu zote vilivyo vyetu.Wengi wet humu ni chadema damu lakini yanapotokea maswala kama haya tunaacha uchadema na kuona tunailindaje nchi yetu kama wajibu wetu wa msingi kabisa.hivi unadhani watu kama Zitto Kabwe wataku-support na upuuzi wako.Tena unaharibu taswira ya chama chetu cha nguvu ya umma Chadema kwa ktudhalilisha mbele ya watu kuwa hatuna uzalendo kama ni kitu cha kwanza kwa mtanzania no matter what! Nikuulize tena hivi umeona jinsi wamarekani bush na obama walivyokutana pamoja kuwakumbuka wale watu waliokufa na bomu kwenye ubalozi wao dar es salaam.BORA UACHE KU-COMMENT VITU USIVYOVIJUA KULI SABABU HUWEZI SIASA UNASHABIKIA HADI UNAHHARIBU MAANA ,yani wewe ni -------- kwelikweli
 
hivi wewe ulitaka jamaa wakae kwenye makambi yao bbaada ya kutoka depo na vyuo mbalimbali nchini na duniani kote bila kufanya practical ?duh hoja nyingine zinanitia unyonge kweli
 
Jamani hata RIP hamtoi. Mabandidu nyie?
Rip maafande wetu
Afadhali yako ndg yanguTripo9 maana hawa jf wengine nawashangaa kbs hata uzalendo kwa nchi yao hawana. wao kukicha wanawaza uchadema na uccm tu.inasikitisha sana kizazi hiki. hivi nyie kweli mnaweza kuilinda nchi yenu nyie! Ingekuwa kafa mwana bongo flavor au bongo movie, ungeona comment za RIP, lkn kwa hawa watetea taifa na amani duniani wanaoneka ni kama mbwa tu wamekufa. nyie vijana wa chadema hamfai kabisa hata kwa kulumagia. naomba nieleweke kuwa mm sina chama. chama changu ni Tanzania
 
Back
Top Bottom