Wanajeshi hawa kweli ndo hivi?

Wanajeshi hawa kweli ndo hivi?

SABABU KUMI NA MOJA ZA KUOLEWA NA WANAJESHI.
Malikia Elizabeth amepata kusema hivi "kama utampenda mwanajeshi, nyanyua glasi ya mvinyo juu, na kama Mwanajeshi akikupenda wewe nyanyua kichwa chako na tembea kwa madaha kama malikia.
Wajeda wanasema hivi...
1. Uaminifu uliotukuka
Tumejidhatiti kuitumikia nchi yetu na uaminifu juu ya nchi yetu ni wa hali ya juu. Hua tunatimiza viapo vyetu kwa vitendo. Hivyo basi hata katika mahusiano tu waaminifu kwa mpenzi mmoja na tunatimiza yale ambayo tuliahidiana.
2. Tu wapole
Kama wewe ni mwanamke na ukafanikiwa kuingia katika kambi ya jeshi, utafunguliwa kila mlango na askari aliyepo. Kama utaangusha kitu ukiwa ndani ya kambi na upo jirani na askari lazima atakusaidia kuokota. Tumekueleza kwamba hatuwezi tukakuacha ulipie dinner? Hii inaonesha ni jinsi gani tulivyo wapole.
3. Tunatumia muda wetu vizuri.
Tunaweza tukakaa kambini miezi sita au muda mwingine mwaka mzima, tunaweza tukaenda kusimamia amani mashariki ya kati na kwingineko. Hivyo basi tunavyopata muda wa kukaa na wapenzi wetu hutumia muda wetu vilivyo.
4. Kuwa nasi ni furaha.
Wanawake wengi hawana mazoea na bastola na silaha kama hzo, mazoez ya kimapambano na mengineyo. Kila uhusiano mpya unavyoanza watu hufundishana mambo mbali mbali, hivyo basi na sisi tutawafundisha kwa utani na bashasha nyingi huku tukifurahi pamoja.
5. Tuna hofu na Mungu
Tumekumbana na mengi sana katika career yetu ya uaskari. Muda mwingine tumekaribia kifo ila tulifanikiwa kukikwepa. Tunajua hatuwezi kukiepuka kifo kwa matakwa yetu bali Mungu ndio anatusaidia. Tunajua ndio anatulinda na kututizama. Sisi ni watu wa dini na tunasali kwa Mungu wetu. Maana Mungu asipoulinda mji wakeshao wakesha bure.
6. Tunajali.
Sisi tunajali sana, tumeshuhudia watu wengi wakipata tabu kwa njaa na vita, ubakaji na maradhi yasiyokwisha. Tunatambua sana thamani ya kuwa na roho nzuri. Siku zote tutaku "treat" kwa kukujali na kuhakikisha kwamba unatambua sekunde yako moja kwetu ni ya muhimu mno.
7. Kwa sababu tubatambua umuhimu wa urafiki, tutakuwa marafiki zako siku zote. Nafikiri mahusiano mengi hufa kwa sababu mtu anakuwa sio rafiki na mpenzi wake. MpenI wako anatakiwa awe ni mtu wa kifurahia nae pamoja, kutoka pamoja, maongezi ya kina pamoja. Tuko vizuri katika hilo.
8. Tunayo Maarifa.
Sio wote tulioenda chuo. Sio wote tuliosafiri maeneo mbalimbali duniani. Ila tunatambua ni nini kinachoendelea ulimwenguni kwa sababu kazi yetu inatuhitaji kujua hilo. Tunafahamu juu ya Islamic State, Taliban, Hezbolah, Boko Haram na Migogoro ya Syria. Tutakufunza mengi kuhusiana na tamaduni, watu na maisha kiujumla. Olewa na sisi hutajuta.
9. Tendo la ndoa.
Sisi sio wazembe katika tendo takatifu la ndoa, tunawatendea haki wenzi wetu kwa kuwaridhisha. Hii inatokana na sisi kufanya mazoezi mara kwa mara hivyo basi kilele chako ni guarantee kabisa kwetu. Mungu akijalia uolewe na sisi utaliona hilo.
10. PHYSICAL AND HOT
Kimwili tupo vizuri, tunanguvu hii inamaanisha kwamba siku zote tegemea ulinzi kutoka kwetu na msaada wa kunyanyua vitu vizito. Kama vile kunyanyua friji, kuhamisha kabati na masofa. Nguvu zetu na muonekano wetu utakufanya ujisikie salama. Tuna 6 packs, 9 packs, 12 packs ni wewe tu kuzitaja.....
11. Kama unataka attention wewe olewa na sisi kwa sababu tumeshazoea kusikiliza oda na kuzitii.
Kupitia sisi mnahakikishiwa usingizi, uhuru na mshikamano.
Msituogope na kututenga,
Ni sisi wanajeshi wote ulimwenguni.

Sina uhakika na statement hii wakuu.
Chezea jeshi wewe huku ni kifaru tuu aliweza kuhimili mziki wake mbwa na farasi walikimbilia !....... hapa sisemi ila wanaojua wameelewa!!!
 
Chezea jeshi wewe huku ni kifaru tuu aliweza kuhimili mziki wake mbwa na farasi walikimbilia !....... hapa sisemi ila wanaojua wameelewa!!!
Hahahaaaa...hapa tutajua tu nani ni mwanajeshi....
 
Kama zile ndege zilizobugudhi watu katika jiji la Dar kwa siku mbili mfululizo ni zenu, futa hiyo namba 2, 5, 6 na 8. Kwa sababu mtu yeyote mwenye sifa hizo ulizoweka hapo, angetambua kuwa katika mji mkubwa kama Dar unaokadiriwa kuwa na wakazi kama milioni tano, kuna watoto wachanga wengi, vikongwe na watu wenye matatizo ya kiafya au wagonjwa ambao siyo utu kuwapigia makelele ya vile!
 
Kama zile ndege zilizobugudhi watu katika jiji la Dar kwa siku mbili mfululizo ni zenu, futa hiyo namba 2, 5, 6 na 8. Kwa sababu mtu yeyote mwenye sifa hizo ulizoweka hapo, angetambua kuwa katika mji mkubwa kama Dar unaokadiriwa kuwa na wakazi kama milioni tano, kuna watoto wachanga wengi, vikongwe na watu wenye matatizo ya kiafya au wagonjwa ambao siyo utu kuwapigia makelele ya vile!
Unaleta UKUTA mpaka huku?....jinga weeee.
 
Wow! Wanajeshi nawapenda jamani, na hizo sifa zote wanazo ndio mana nawapenda zaidi,
Yani ukiwa na mwanajeshi wahisi kabisa ni Malkia wa dunia.
 
Back
Top Bottom