Elections 2010 Wanaharakati watoa masaa 72 kwa serikali......

Hao wanachuo ni wasomi kama wana akili nzuri yakufikiria nakuona mbali walitakiwa kuomba ufafanuzi mapema kutoka tume ya uchaguzi kuwa wao itakuwaje maana tarehe ya uchaguzi ilikuwa inajulikana mapema saana tu.asa wanangoja mambo hadi yaharibike ndio waje wajifanye wanataka haki ya kupiga kura?hao wanzuoni wamechemsha bora wakae kimya tuu.limeshapita hilooooooooo no soln zaidi yakutulia na kumgoja 2015.teh teh teh.

FIKIRIA MARA MBILI MKUU,KUMBUKA TULIKUWA NA UHAKIKA WA KUWAPO VYUONI kuanzia late sept. Kila mwaka,baada ya kufunga vyuo ndo wakatangaza usanii huu. Bodi ya mkopo ni wasanii kwa haki ya watanzania. Wasaidie wanavyuo kukwepa uonevu.
 
Haki ya kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 sio huruma wala kitu cha kuomba ni HAKI! Sioni mantiki ya kutaka kuwazuia wanavyuo kupiga kura! Kwa nini iwe hivi! Kwa manufaa ya nani? Kumnyima Mtanzania yeyote kupiga kura mwenye umri husika mwenye akili timamu ni kinyume na Katiba ya nchi ibara ya 5(1) na ibara ndogo (2). Kwenda kinyume na katiba hii ambayo ni dira kwa Watanzania wote nikuonyesha ni vipi viongozo wetu wasivyo na haya hata kujaribu (kama sio kuthubutu) Kuibaka katiba hii ambayo wao wanaielewa zaidi kuliko watanzania wengi wao wanaoamini kuwa ni maamuma tusioelewa kitu. Imefika mahali Watanzania walio na uchungu na nchi hii wasimame na kusema HAPANA.
Nchi hii imekuwa ikiendeshwa na kikundi kidogo cha watu wanaotaka kutupeleka mzobemzobe wanakotaka wao. Wakae wakielewa kuwa siku za mwizi ni arobaini na sasa zimetimia. Watake wasitake mapinduzi ya kweli yatafanyika kama sio sasa basi hata kesho. Unapozungumzia Mapinduzi hatuzungumzii umwagaji wa damu kama wao wanavyofikiri. Ni mapinduzi ya kupiga kura kuwaondoa madarakani. Na hili linawezekana. Wote kwa pamoja tukisimama imara na kukusema tunataka mabadliko ya nchi tunaweza and that begins with YOU!
 
Hawa siyo WANAHARAKATI,bali ni wavurugaji . Kama ni wanaharakati kwa nini hawadai haki ya makundi mengine ya watu ambao kwa namna moja ama nyingine wanaweza kukosa kupata fursa ya kupiga kura hata kama walijiandikisha: 1.Kwa nini hawadai haki ya wagonjwa ambao watakosa fursa ya kupiga kura kutokana na wao kuwa hospitalini? 2. Kwa nini hawadai haki ya wasafiri ambao watakosa fursa pia ya kupiga kura kutokana na wao kuwa safarini?

Kwa nini hawa wanaojiita wanaharakati wamelilenga kundi moja tu la wanafunzi wa vyuo vikuu na kuacha makundi mengine ya watu? HAWA NI WANASIASA TU WALIOVAA NGOZI YA WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU. WANAHARAKATI WA KWELI HAWABAGUI MAKUNDI YA WATU
 
Sijui ni mimi tu...kwa kweli sijaona point hapo!
1. Nani kakwambia mgonjwa haendi kupiga kura? na ulitaka mgonjwa wa ICU pale KCMC atokeje kwenda kupiga kura!??ama aliye kwenye coma!?? Somethings, ni matokeo haupangi yawepo..ikatokea nimelazwa siku ya kupiga kura sijiwezi kabisa..basi Mungu anajua mipango yake. Kama nina kanguvu fulani basi nitajikongoja kwenda kupiga kura..

2. Naomba nisikujibu...

**Tungekuwa na online voting system haya yote yasingekuwepo. Maana, it would have allowed everyone to vote wherever they are! Lakini hii ndo bongo...tunaenda tu hivyohivyo!!!! na Mungu atusaidie...

Nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza...
 
Back
Top Bottom