Wanaharakati watishia kuzuia uchaguzi 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati watishia kuzuia uchaguzi 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kubwajinga, Feb 18, 2010.

 1. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wanaharakati watishia kuzuia uchaguzi 2010

  Na Richard Makore; 17th February 2010


  [​IMG]
  Mkurugenzi wa LHRC, Francis Kiwanga


  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kinatarajia kwenda mahakamani kusimamisha Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, 2010 ikiwa serikali itakaidi kubadilisha vipengele vya sheria na kuweka mazingira mazuri ya kuruhusu mgombea binafsi.

  Kadhalika, kituo hicho kimekerwa na kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, kwa kutangaza kuwa serikali haitambui kuwepo mgombea binafsi.

  Msimamo huo wa LHRC ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wake mkuu, Francis Kiwanga, alipozungumza na waandishi wa habari.

  Alisema Mahakama Kuu ilishatoa hukumu mwaka 2006 na kutamka kuwa mgombea binafsi anaruhusiwa na kwamba kitendo cha serikali kudharau amri hiyo ni kosa kisheria.

  Alisema ndani ya miezi minne lazima serikali ihakikishe inarekebisha vipengele vya sheria vinginevyo watakimbilia mahakamani ili kupinga uchaguzi usifanyike bila mgombea binafsi kushiriki.

  Alisema kuna sheria nyingi zilizowahi kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge katika kipindi kifupi hivyo hatua ya kuruhusu mgombea binafsi inawezekana.

  Alitolea mfano wa sheria ya uchaguzi ambayo ilijadiliwa na wabunge na kupitishwa ndani ya siku mbili.

  Alisema hukumu ya Mahakama Kuu haijatenguliwa na Mahakama ya Rufaa kama alivyosema Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani hivi karibuni.

  Kiwanga alisema serikali inakataa kwa makusudi amri halali ya Mahakama na kwamba ubabe wake huo unakinzana na kifungu cha 14(3) cha Sheria ya utekelezaji wa haki za msingi za binadamu.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wazo zuri la kupigania. Tuombe Mungu wasije wakawa ni vibaraka wa JK.
   
 3. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 463
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kubwajinga mbona hatukuelewi?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...