Wanaharakati tuwe na ujasiri - Moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati tuwe na ujasiri - Moshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mendelian Inheritanc, Jan 9, 2012.

 1. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CDM Kata ya Segerea Jeff Moshi amewataka wale wote wanaopigania haki katika nchi hii, wanafunzi vyuo vikuu,walimu na wafanyakazi sehemu mbalimbali, madaktari pamoja na wanaharakati wanaopinga ufisadi,anawatia moyo kwa kuwakumbusha kile alichowahi kukisema Mandela “Popote pale hakuna njia rahisi ya ukombozi, na wengi wetu itabidi tupitie tena na tena kwenye bonde la uvuli wa mauti kabla ya kufikia kilele cha mafanikio” Aidha mwanafalsafa wa Morocco, aliyefia Zanzibar mwaka 1313 alisema “Tutakapokufa msitutafute kwenye makaburi yaliyopambwa kwa kupakwa chokaa, bali tutafuteni kwenye mioyo ya watu tuliowatumikia”
  Aidha, wapo watanzania wanaokemea maovu, lakini wanakumbana na vitisho.Wanaharakati hawa pia wasikate tama, kwa kuwa kama alivyosema mwanafalsafa wa ujerumani, Arthur Schopenhauner (1788-1860), “Ukweli wowote hupitia ngazi tatu, kwanza, ngazi ya kukejeliwa, pili ngazi ya kupingwa na hata ikibidi kumwaga damu, na tatu, kukubalika kwa kuwa ukweli hujisimamia wenyewe”
  Vilevile, watanzania tubadilike tuondoe woga, Tunatakiwa tuwe na ujasiri.Mwanamama mpigania haki wa Burma Aung Suu Kyi alipotoka gerezani alipokuwa amefungwa kwa kupigania haki alisema “gereza pekee na la ukweli na halisi ni woga, na uhuru pekee wa ukweli na halisi ni uhuru dhidi ya woga. Mwenyekiti huyo wa BAVICHA Segerea aliyazungumza hayo jana. Nawasilisha!!!!!!
   
 2. p

  pilu JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona Umejipanga kweli kweli mkuu,sijui umetumia siku ngapi kuianda hio mada ,kila lakheri mkuu!
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Kilalakheri chadema kwa nia ya dhati kabisa la kulikomboa nchi hii mikononi mwa mafisadi!
   
 4. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ccm wanapaswa kufanya kazi ya ziada ilikurudisha imani iliyopotea kwa wa tz otherwise should get prepared to become an oppostion political party
  no sooner,cdm hawaonyeshi kabisa kukata tamaa na matunda ya maandamano yao na mikutano vilivyokuwa vikibezwa sana yanaonekana dhahiri raia wanaonyesha wazi na kupaza sauti kuwa wanataka mabadiliko na haki zao na hawaogopi tena vitisho na ninatabiri mwaka huu cdm itaimarika na kuenea sehemu nyingi zaidi kuliko kipindi chochote coz wameunza mwaka kwa kasi mno
   
 5. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  kila anachoongea hata katibu kata wa chadema au kiongozi wa tawi la wakereketwa wa chadema mtatupostia humu----
   
 6. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tutapost tu mradi kiwe na itikadi za ukombozi wa taifa hili na maslahi ya kuelimisha umma wa watz kadogooo
   
 7. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumekucha vijana msilale kwani bado mapambano yanaendelea
   
Loading...