Wanaharakati Mafia watishia kuishtaki Serikali na DC!

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,275
391
Wanaharakati Kisiwani Mafia wamedhamiria kuishtaki serikali pamoja na DC wa wilaya hiyo endapo sheria itakiukwa kwenye kushughulikia malalamiko ya wananchi wilayani hapa. Hayo yameelezwa leo pale wanaharakati hao walipokutana na wananchi ambao walikuwa wakilalamika juu ya ubaguzi wa sheria kwa viongozi wa serikali na raia wa kawaida.
Hayo yametokea pale Hifadhi ya Bahari Mafia kukamata boti za uvuvi za DC wa mafia zikivua ndani ya Maeneo ambayo yamehifadhiwa(maeneo tengefu) na kushindwa kuchukuliwa hatua kwa wahusika ikiwemo kumfikisha mahakamani mmiliki wa boti na mitando ya kuvulia ambaye ni DC. Wananchi hao walielezea kusikitishwa kwao na kitendo hicho na kusema ya kwamba, wananchi kadhaa walishikwa na makosa kama hayo, mali zao ikiwemo maboti ya uvuvi, nyavu na mitumbwi yao kutaifishwa na kuchomwa moto na mamlaka husika. Na kushangazwa na kitendo cha mkuu huyo ambaye alitakiwa kuwa mfano na msimamizi wa kuhakikisha maliasili inatunzwa. Baadhi ya wavuvi ambao wameajiriwa na DC huyo wameeleza kwamba, wao wamepewa baraka zote kutoka kwa mwajiri wao juu ya kuvua maeneo hayo ya hifadhi na kuwaahidi atawalinda na lolote litakalotokea. Hivi sasa DC huyo ameanza kutoa vitisho kwa baadhi ya Wafanyakazi wa hifadhi ya bahari walioshiriki kwenye oparation hiyo ilifanikiwa kukamata wavuvi haramu akiwemo DC. Baadhi ya staff wa Marine park wamesema wapo tayari kuacha kazi endapo watalazimishwa kuachia nyavu za mkuu huyo ziendelee kuvunja sheria wanazosimamia huku wakiwa wameshiriki mara kadhaa kuchoma nyavu zilizoshikwa kwa makosa yanayofanana na hilo! Huku wakisistiza ya kwamba kama dharau na ubababe wa DC huyu basi akaufanyie huko huko na si kwenye rasilimali za bahari ambazo wameapa kuzilinda kwa nguvu zao zote na hawatatishwa na mtu yeyote kwenye kutekeleza majukumu yao ya kisheria.
Wanaharakati kwa upande wao wamedhamiria kuishtaki serikali kupitia mamlaka hiyo ya uhifadhi endapo itashinda kumchukulia hatua za kisheria DC huyo na kufanya hivyo kwa wananchi masikini na wanyonge!
 
Mheshimiwa Membe tafadhali

njoo Mafia umchukue huyu DC wako mpeleke huko kwenu sisi tushamchoka

uvumilivu unamwisho wake

its never too late
 
Kwa taarifa nilizozipata ni kwamba, DC jana aliwaita baadhi ya marengers walioshiriki kukamata nyavu zake na kufanya nao mahojiano kwa saa kadhaa, na kuwatisha kwamba iwapo hawataachia mali zake hizo basi atahakikisha kazi zao ninakuwa mashakani kama alivyofanya kwa mwenzao mmoja ambaye alimsimamisha kazi zaidi ya mwaka mmoja kinyume cha mamlaka!
 
Mangochie anapenda ku manage kwa kutumia vitisho na hizi kashfa za ufisadi na matumizi mabaya ya pesa sidhani kama zitamsaidia

bila kusahau tuhuma ya kuuza shule ya wananchi kwa wazungunu
 
Back
Top Bottom