Wanaharakati acheni uwongo sasa.

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
168
Reaction score
281
Tunajua mnapambania ugali wenu ila hii vita yenu na serikali ni ya hovyo.

Kwa sasa mnasema waliouwawa ni 10,000 kutoka elfu moja ( 1000) mnadhani binadamu ni sisimizi. Idadi hii hata kwa kiziwi tayari ni siasa chafu.

Pili, Tanzania ni wazi sana tunaomba watu waliopigwa risasi nyumbani kwao watoe taarifa kwa hiyo CNN acheni kupotosha kwa jeshi lilienda kuuwa watu nyumbani.

Kwa harakati hizi naona kuna chama kilihusika moja kwa moja katika machafuko.

Rais hausiki na mauji na ndiye rais bora sema siasa uchwara ili wafanya vijana watumiwe kama chambo.
 
Pili, Tanzania ni wazi sana tunaomba watu waliopigwa risasi nyumbani kwao watoe taarifa kwa hiyo CNN acheni kupotosha kwa jeshi lilienda kuuwa watu nyumbani.

Upo ushahid wa video na pia ushahidi wa vifo vilivyotokea mtu akiwa nyumban kwake na akapigwa Risasi.

Kwahiyo kuna washenz walikuwa wakiona mtu anachungulia tu nje au anachukua video wanamlenga kama wako kwenye Game.

According na Wikipedia. Vita ya kagera iliua watu karibia elfu 5.
According na Warioba . Mauaji ya tar 29 yalizidi mauaji ya Vita ya kagera.

Kwahiyo usituhumu sana wanaharakat. Angalia chanzo 😎😎😎😎.
Kama Serikal ina chanzo cha kusema idad kamili ya vifo. Basi waseme. Tuachane na kuamini ya Warioba.
 
Nashukuru watu mmeanza kuamka wamebaki nyumbu wachache jf ambao akili zao wamefungia kabatini wanatumia za kigagula Mangekimambi, kila siku wanakuja na idadi mpya mara elfu 10 mara elfu 23 ilimradi kila nyumbu karusha teke.

Amani ya nchi hii italindwa kwa gharama yoyote iwe iwevyo ukileta uhalifu wa kinyumbu kuiba na kuharibu mali utashughulikiwa kwa kupelekewa moto mkali bila chembe ya huruma haijalishi mtakua nyumbu elfu 20 au laki 3 wote mtalionja joto la jahanam.

Hakuna huruma kwa nyumbu wahalifu
 
Idadi umeipinga kwa data zipi? Idadi yako wewe ni ngapi na umeipata wapi? Rais hausiki kivipi kwani kuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kutoa amri ya 'shoot to kill'? Mbona kwenye hotuba yake na vile vizee vya CCM hakukanusha kutoa amri ya hiyo badala yake aliitetea kuwa ilikuwa ni reasonable force to contain the demonstrators? Watu wanaolia mpaka leo kukoso miili ya ndugu zao mnawaambia nini? Una habari kuwa Songwe huko watu waliokimbilia Milimani for almost a week baada ya watu kuanza kugongewa milango na kupigwa risasi majumbani? Clips za watoto under 14 na mwanamama aliyepigwa risasi ya mgongo akiwa mjamzito who is supposed to take the responsibility for the atrocities/killings? Haya mambo this time around hawataweza kuyafukia kirahisi kama walivyozoea, uuaji na unyama uliofanyika lazima viongozi wakiri na kuomba msamaha hadharani, wahusika lazima wachukuliwe hatua, uchunguzi ufanywe na watu wasio connected na dola wala chama tawala.
Viongozi wa TZ hawajazoea raia kuwauliza maswali magumu ndiyo maana wanateka tu na kuua.
 
Shekh sharif mwenyewe anajilaumu kubaki nyumbani
 
Basi semeni mliua wangapi, na mliwapeleka wapi.
 
Mkoa wa dar es Salaam peke yake wamefika na kuvuka watu elfu...maiti azikupelekwa mochwari tu zilikuwa zimekusanywa sehemu nyingi na mapolisi, zilizo pelekwa mochwari ni wale walio fia mahospitalini ...ambulance zilikuwa azichukui maiti mitaani bali majeruhi hivyo mahospitalini walio lundikwa mochwari ni wale walio kata roho wakiwa kwenye harakati za kukimbizwa hospital na walio fia hospitalini ....Kumbuka kuwa haya mauaji yalikuwa mikoa mingi tena sehemu mbalimbali hadi vijijini.
 
Wewe uliyekuwa umefungiwa ndani unaangalia TBC tuambie ni wangapi.
 
Acha tishatisha watu.
 
Hata kama walikufa kumi au mmoja lazima wahusika wawajibike, uhai wa mtu huwezi ukaudhulumu kirahisi hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…