Wanahabari wa Arusha acheni UABUNUWASI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari wa Arusha acheni UABUNUWASI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Las Mas Bobos, Sep 12, 2012.

 1. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimeshangazwa na upole-uzembe wa wanahabari wa Arusha kwa kitendo chao cha kukubaliana kiulaini na jeshi la Polisi kusitisha maandamano yao kwa sababu za KIUABUNUWASI. Ikiwa waliamua kuandamana si ni lazima walikuwa na malengo? Sasa dhana ya maandamano ilikuwa na maana gani kwao?

  Navyofahamu mimi, watu huandamana kama njia ya kupaza sauti zao kwa pamoja. Nia ya KUPAZA SAUTI ni kutaka KUSIKIKA. Ujumbe wa mabango kelele na nyimbo na ku-draw attention ya walio mbali na karibu wapate kusikia kinachowaliza. Na kwa jambo kubwa kama hili ambalo limeiumiza nchi ktk mazingira haya ambayo mlalamikiwa ndio huyo huyo mtoa maamuzi, tulihitaji kuwafikia wengi zaidi hadi nje ya mipaka yetu ili nao wajue maswahibu yetu.

  Cha kushangaza, wao pamoja na Jeshi Tuhumiwa wakafikia makubaliano kwa sababu ya UGENI. Ugeni huu kwa maoni yangu, ndio hasa ulikuwa wakati muafaka wa kufanya maandamano. Kama wageni hawa wanatoka nchi mbali mbali, basi maandamano yangefanikiwa zaidi kwani yangesikika mbali zaidi na wao wakayajua matatizo yetu, wakaona dhuluma hii tunayofanyiwa na serikali yetu.

  Mimi nachoona ni kuwa haya yalikuwa maandamano ya kinafiki. Wenzetu huvizia ugeni kuandamana, sisi tunakubali kuahirisha maandamano kupisha ugeni. Hiki ni kichekesho. Wenzetu huvizia mikutano mikubwa kama ya G8, WES n.k kunyanyua mabango yaonekane lkn sisi tunaweka ya kwetu chini kupisha ugeni, JE, TTULITAKA KUMUONESHA NANI KAMA SI HAO WAGENI?

  Kama kuna mtu anajidanganya kuwa anaandamana kuifikishia ujumbe serikali hii kiziwi basi huo ndio uabunuwasi ninaousema. Hii si serikali ya kuelezwa kwa hapa ilipofikia, ni serikali ya kushtakiwa kwa washirika wake.

  Walichokifanya wanahabari wa Arusha ni sawa na kubandika tangazo USIKOJOE HAPA na kulibandika chumbani kwako ambako unaishi wewe mwenyewe.
  Kama maandamano yenu hayahitaji kusikika, hiyo siku mtakayoandamana mtaandamana ili iwe nini?
   
Loading...