Wanahabari tuisaidie nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari tuisaidie nchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KGARE, Aug 3, 2012.

 1. K

  KGARE Senior Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ifikie wakati sasa tuombe vyombo vyetu vya habari kama ITV, STAR TV, TBC, CHANNEL 10, CLOUDS TV, SIBUKA, na Vyombo vingine kama radio na Magazeti..,KUANZISHA HOT INTERVIEWS kwa Viongozi Wetu wa Nchi. Ambapo mada Motomoto za maslahi ya Taifa mfano ardhi, ajira,utalii, viwanda, biashara, madini, mashirika/kampuni za kitanzania, maliasili, Utawala bora, n.k ziwe zinawekwa na wanamhoji Kiongozi huyo tena wakiwepo walau Wawakilishi wa Umma wenye ufahamu walau 2 hivi (mfano Wahadhiri, Wanaharakati, n.k).

  Viongozi wawe wanajiandaa kuwaeleza Watanzania na baada ya Kipindi Kiongozi huyo aseme wazi maoni ambayo atayachukua kuyafanyia kazi na alete feedback baada ya Kipindi Fulani.
  Mimi sifurahii na vipindi vya baadhi ya Televisheni vinamleta Kiongozi wa Nchi vinamuuliza maswali binafsi tu na ya kujifagilia au ya kichama tu badala ya kuzungumza mambo Mazito yanayorudisha nchi nyuma ili serikali ifanyie kazi.


  HII NI NJIA MOJAWAPO KWA WANANCHI NA VIONGOZI KUWAJIBIKA KWA NCHI YAO!!
   
 2. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Wazo zuri.Lakini je, hao wanahabari wenyewe wapo? Au unamaanisha hawa hawa wanaoambiwa leteni maswali wanakusanya fasta hata kabla hawajasikia anachokiongea msemaji wanayetaka kumhoji? Hawa hawa walioitwa hotelini na "mmiliki wa dowans" akawaamrisha wasimpige picha wakatii amri hiyo haramu kutoka kwa mgeni? Nchi inamegwa na Malawi kule Ziwa Nyasa, wao wanafurahia juisi tu. Gazeti Mwanahalisi limefungiwa kwa muda usiojulikana bila kuelezwa ni habari ipi iliyokiuka maadili kwa mujibu wa sheria, lakini wamenyamaza kimya kama vile hakuna kilichotokea. Wanauza uhuru wao wa habari kwa bahasha ndogo za kaki. Kwa kifupi ndugu, wazo hili uliloleta haliwezi fanikiwa kwakuwa Tanzania hatuna wana habari. Tuna mfano wa wanahabari ambao si mbaya kama tukiwatafutia jina jingine.
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mi hakuna waziri hata mmoja nataka kumsikia sasa hivi. Kwanini tukae chini nakuskiza wezi wakiongea kwenye tv
   
 4. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sio sasa hivi kwa waandishi wanaojipendekeza, a.k.a buti likazi teh he he...
   
 5. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanahabari wenyewe wooga kuna yule wa TBC sijui anaitwa nani hata hajijui!
   
 6. m

  markj JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  wanahabari wenyewe wakina KIBONDE, HANDO, DIDA WA MCHOPS,SAKINA LIYOKA, CASTRO DICKSON, sijui FEIZA, KWISA! hahaha watazidi kutupoteza tu, mana watakuwa wanataka kuuza sura na kujipendekeza kwa hao wahusika! ninamashaka na waandishi wa habari za hapa nchini!
   
 7. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu tatizo kubwa ni ukuu wa wilaya!
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  anaitwa zacharia...marine hassan ana ujasiri wa kuwatetea mafisadi
   
 9. m

  markj JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  sasa kajamaa kama kale ka kibonde kakipewa ukuu wa wilaya si wilaya itavunda kama akili zake zilivyovunda! Hando je? Ndo kabisaa box! Elimu muhimu mkuu!
   
 10. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni sahihi nami naunga mkono hoja tayari ITV,STAR TV ,CHANEL 10 wameanza tuwasapoti , lkn TBC na CLOUDS hizo ni ofisi za chama flani sio vyombo vya habari
   
 11. D

  Davie Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Umemjibu huyu bwana vizuri kabisa...hao wanahabari ni wepi...?
  Wa kuambiwa kutuma maswali.., ni wale wa kudubiria labda neeema za u DC...
  Hamna kitu hapo..
   
 12. K

  KGARE Senior Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Duh...Sasa kama kila njia ya kuliondoa Taifa letu kwenye janga la umasikini inakwama.Sasa si tutajuta kuzaliwa hapa!! I pray that the day comes when Tanzanians will feel proud of their Country and Leaders.
   
 13. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu huyu jamaa ni hatari kuhoji tuu anakuwa kama anataka kulia hivi yaani hayupo happy na kazi yake, ni mwoga sijapata kuona, hata wanayoongea wengine yeye anaogopa!
   
Loading...