kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,785
- 20,164
Jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah, limezindua kombora jipya la balestiki la masafa ya kati la Qahir M2.
Televisheni ya al-Masira ya Yemen imenukuu taarifa ya kikosi cha mizinga cha jeshi la nchi hiyo ikisema kuwa, baada ya mafanikio makubwa ya ufyatuaji makombora matatu ya balestiki ya Qahir M2, yaliyoshambulia kwa kulenga shabaha kambi ya kijeshi ya 'Malik Khalid' ya Saudia, katika eneo la Asir kusini magharibi mwa nchi hiyo, sasa imezindua rasmi shughuli za kombora hilo.
Kombora hilo la balestiki lina sifa ya kushambulia umbali wa kilometa 400, kichwa chenye uzani wa 350 na uwezo wa hali ya juu wa kulenga shabaha kati ya mita tano hadi 10. Ripoti ya jeshi la Yemen imeongeza kuwa, uundwaji wa kombora hilo, umejiri katika fremu ya juhudi kubwa zenye lengo la kuinua uwezo wa makombora wa jeshi la nchi hiyo, kukabiliana na hujuma za adui na kadhalika kulinda umoja na uhuru wa Yemen. Itafahamika kuwa, uwezo wa kiulinzi wa jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah, umeimarika katika hali hali ambayo taifa hilo limewekewa mzingiro wa kila upande wa utawala wa Saudi Arabia na nchi waitifaki wake.
Saudia kwa kushirikiana bega kwa bega na Marekani, Israel na baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati na nje ya eneo hili, ilianzisha hujuma zake za kila upande huko Yemen, mwezi Machi mwaka 2015, kwa lengo la kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kukimbilia mjini Riyadh. Mashambulizi hayo hadi sasa yamesababisha mauaji ya zaidi ya watu elfu 11 wa Yemen, makumi ya maelfu kujeruhiwa na kuwafanya mamilioni ya watu kuwa wakimbizi, sambamba na uharibifu mkubwa wa miundomsingi ya taifa hilo masikini la Kiarabu.
My take; hahaa naona imekua fashen kuzindua kombora
Media nyingine bhana
hahaaa