Wanafunzi Wasomea Chini Ya Miti Dar...

JK ana mpango wa kuwapa laptop hao walimu wote kufikia mwaka 2015. Pia ana mpango wa kuhakikisha kila shule ina kompyuta ifikapo 2015. Nafikiri atakuwa anaziweka humo chini ya miti. Haya yatakuwa ni maendeleo makubwa sana nchini.
 
Shule utafikiri NAZI concentration camp.There ought to be laws against these abuses. Hivi unategemea hawa wanaafunzi watakuwa watu wa kawaida kweli ? No wonder tunapataa marais Vikwete
 
Hivi wazazi wa watoto hawa wako wapi? How do you let your child go to a school looking like that? Unawezaje kuwa na amani kuwa mwanao is safe wakati hali halisi ndio kama hiyo. Kama wanaisubiri serikali kukarabati hiyo shule watasubiri sana, kwani ata wapinzani wakiingia madarakani hawatakarabati shule. Kama jamii inabidi tuwajibike na kubadilisha mazingira yetu, serikali haiwezi kutufanyia kila kitu. Tukiwa pro active itakuwa rahisi kuiwajibisha serikali kwani tutakuwa na mifano.
 

labda ungejiuliza uwezo wa hao wazazi......i guess wangekuwa na uwezo wangewapeleka "st.academy school".....
 
Kama Mkuu wa kaya akifuta ziara za kitalii kwa mwaka mmoja nchi nzima inakuwa na madarasa na madawati ya kutosha

Lakini bahati mbaya hayo hayako katika priorities zetu
 
Hayo ndiyo MAISHA BORA yanayohubiriwa majukwaani kila kukicha. Hali kama hiyo iko DSM ambapo viongozi wote wa Taifa wamejilundika, ukisogea mikoa ya pembezoni kidogo utakayoyaona kama una roho ya huruma utaanza kulia kabla hujaelezwa chochote. Najaribu kufikiria pale Rais aliposema kwenye hotuba yake kuwa anashangaa jinsi mambo yalivyobadilika na kuwa ktk ziara zake mikoani kila anapopita wananchi wamejaa furaha tele kutokana na maendeleo yaliyopatikana hususan ktk kipindi cha awamu ya nne ya uongozi wake.

Wananchi wanatakiwa kufikiria kwa kina na kuangalia uhalisia wa mambo yanayotendeka ktk jamii na kuwa makini zaidi na maneno yanayotolewa na viongozi waliopewa jukumu la kuongoza taifa letu.
 

inaonesha jinsi ilani ya ccm ilivyotekelezwa. Hatudanganyiki 2010
 
Kwa tulivyo wachoyo na wabinafsi akija kutokea mmoja wa hao watoto akawa mkubwa serikalini hatakumbuka (atasahau jumla), sioni kama ni KKT tu wa kumlaumu hapa, hao hao kina Dr Sl tutawapigia na incase wakishinda (hatutegemei anyway) mambo yatakuwa yaleyale tu.
 
NN hivi tutachangia mangapi na sisi tuna ukata kibao? Hapa naomba nipishane na wewe mawazo!
Hizo kodi zetu wanazotanulia hawa wezi kweli nitapat wapi courage ya kuchanga wakati mtu anachota 300 b na kuondoka na anatanua kwa matusi tu mengi huko mtaani?
Mimi ni mmoja kati ya watu wanaochangia sana shughuli za maendeleo hasa kwenye eneo langu. Lakini kwa pesa ya nchi hii inavyochezewa nasita kuendelea kuchangia.
Angalia wenzetu wazungu wametuchangia kiasi gani na kimetutoa tulipokuwa kiasi gani? yaani mpaka sasa wao nao wanajiuliza kuwa pamoja na misaada yote tunayopata mbona hatusogei? No, nadhani kuna shida mahali fulani! Tukianza kufikili kila kitu wananchi watachangia kwa kuwa serikali ime-prove kushindwa tutashindwa kwenda mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…