Wanafunzi washinda rufaa Bodi ya Mikopo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi washinda rufaa Bodi ya Mikopo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 9, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,665
  Likes Received: 82,492
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi washinda rufaa Bodi ya Mikopo
  Basil Msongo
  Daily News; Saturday,March 07, 2009 @20:10

  Wanafunzi 70 wa vyuo vikuu kati ya mamia waliokata rufaa kupinga uamuzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuwakopesha kwa kuzingatia uwezo wao kiuchumi, wameshinda rufaa hizo hivyo watakopeshwa kwa asilimia 100. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema taarifa za wanafunzi 350 zitahakikiwa zaidi kabla ya kutoa majibu ya rufaa zao.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo, imetuma orodha ya matokeo ya rufaa hizo katika vyuo saba vya umma, hivyo mwanafunzi aliyekata rufaa asipoona jina lake kwenye orodha hizo, afahamu kwamba rufaa yake imetupwa na kwamba ataendelea kuwa katika daraja la mikopo alipo sasa.

  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Hamisi Dihenga, alisema katika taarifa hiyo kuwa, matokeo ya rufaa hizo yametumwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Mkwawa, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Ardhi, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Stadi za Biashara Moshi.

  “Kwa waliowasilisha rufaa zao kutoka vyuo vingine nje ya vilivyotajwa hapo juu matokeo yao yanapatikana Idara ya Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, makao makuu, Dar es Salaam,” alisema Dihenga. Novemba mwaka jana wanafunzi wa vyuo vikuu saba vya umma waligoma wakipinga Sera ya Uchangiaji Elimu ya Juu, hali iliyolazimu vyuo kufungwa na wanafunzi wakapewa masharti waliyopaswa kuyatimiza ili waruhusiwe kurudi vyuoni.

  Wanafunzi walilalamika kuwa matokeo ya kipimo hicho hayakuwaridhisha na Wizara iliwataka wakate rufaa kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. HESLB ilianza kutumia utaratibu wa kuzingatia uwezo wao kiuchumi kuanzia mwaka wa fedha 2006/2007 na wanafunzi wote wakapata mikopo kwa asilimia 60, mwaka wa fedha 2007/2008 mikopo ikaanza kutolewa kwa madaraja sita. Daraja A wanakopeshwa kwa asilimia 100, B asilimia 80, C wanapata kwa asilimia 60, D asilimia 40, E wanakopeshwa kwa asilimia 20 na daraja F hawakopeshwi.

  Januari mwaka huu, bodi ilisema katika mwaka huu wa fedha inatarajia kutoa mikopo kwa wanafunzi 60,000 kwa kuzingatia bajeti iliyopangwa ya Sh bilioni 117. Kwa mujibu wa bodi hiyo iliyoundwa kwa Sheria namba 9 ya mwaka 2004, vigezo vinavyozingatiwa katika kupanga madaraja hayo ni historia ya elimu ya aliyeomba mkopo, kiwango cha elimu ya wazazi au walezi wake, shughuli za kiuchumi za wazazi au walezi wake, mali za mwombaji na wazazi au walezi wake na mahali zilipo.

  HESLB imetaja vigezo vingine kuwa ni hadhi ya maisha ya mwombaji na hadhi ya maisha ya wazazi au walezi wake katika jamii na hali ya kijamii ya mwanafunzi aliyeomba mkopo kama vile yatima au mwenye ulemavu. Januari 21 mwaka huu, bodi hiyo ilisema wanafunzi wengi walioomba mkopo kwa ajili ya masomo ya mwaka wa kwanza 2008/2009 wapo katika daraja B, hivyo watakopeshwa kwa asilimia 80, na pia asilimia 52.66 wanaoendelea na masomo wengi wapo daraja B hivyo watakopeshwa kwa kiwango hicho.

  Wanafunzi wanakopeshwa kwa asilimia 100 wanapata fedha hizo kwa ajili ya chakula na malazi kwa idadi ya siku atakazokaa chuoni, vitabu na vifaa vya kuandikia, utafiti, na wengine wanaokopeshwa ili walipe ada ya mafunzo, walipie mahitaji ya kitivo na wanapata pia fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo muda huu wakati rufaa zao zinasikilizwa wanafunzi hawa walikuwa wapi? Je walikuwa wanahudhulia masomo au walikuwa wanasubiri rufaa zao? kama walikuwa hawahudhulii masomo je watarudia mwaka au inakuwaje hapa sijaelewa kidogo. Kunafidia yoyote kwa hawa wanafuzi maana nadhani iliwagharimu pesa kukata rufaa.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huu utaratibu wa ''Means testing'' hauko makini katika kutoa matokea yake ya mwanafunzi yupi apewe asilimia ipi.......! Naamini kuna wanafunzi wengi tu ambao wangestahili kupata 100% lakini wanapata chini ya hapo na wapo wanaopata 100% wakati hawastahili kwa maana wazazi au walezi wao etc wanauwezo wakuwalipia gharama zote za shule.

  Mimi kwa mtazamo wangu uamuzi wa kubagua nani apewe kiasi gani unatakiwa uwe reviewed critically ili ulete maana zaidi kuliko sasa, ambapo need students hawasaidiwi ipasavyo kwa sababu either kukosa taarifa zao zilizo sahihi au kutokana tu na watendaji wa bodi kukosa umakini katika kuchambua taarifa wanazopewa na wahitaji.
   
Loading...