Wanafunzi Wanafeli kwa Uzembe wao - Waziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Wanafeli kwa Uzembe wao - Waziri

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kibogo, Oct 5, 2012.

 1. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema kufeli kwa baadhi ya wanafunzi hakutokani na walimu kutokamilisha mitaala bali kutokana na uzembe wa wanafunzi wenyewe, waziri alitoa kauli hiyo jana 04.10.2012 jijini Dar alipokuwa akitoa taarifa kuhusu mtihani wa kidato cha nne na mtihani wa maarifa inayotarajiwa kuanza Oct 8 – 25.
  Kwa kauli yake amesema wanafunzi wanaotoa madai hayo wengi wao ni wale waliokuwa wakishindwa kuwasikiliza walimu wakati wakifundisha darasani na alisema kwa kawaida mfa maji aachi kutapatapa hivyo hao wanaosema kwamba walimu hawamalizi mitaala mara nyingi ni wale waliokuwa wakipata sifuri tangu awali.

  My Take.
  1. Hivi huyu naibu waziri anajua anachokisema au anaonge kwa sababu watoto wao hawasomi shule za mchangani?

  2. Tumeshuhudia mgomo wa walimu ambao serikali imeshindwa kutekeleza madai yao ya msingi, hivyo walimu watakuwa wanafanya kazi ipasavyo? Kama sio je watamaliza mitaala katika kufundisha hata kama watamaliza je watafundisha ili mwanafunzi aelewe au bora kipindi kiishe?


  3. Tumeshuhudia matokea ya Form 4 mwaka jana 89% karibia na 90% walifeli inamaanisha amekwisha sahau matokeo hayo na je serikali inajua sababu ya kufeli huko kwa hao wanafunzi?

  4. Shule nyingi za kata zimejengwa lakini nyingi zina walimu wasiozidi 3 je wanaweza kufundisha ipasavyo? Na anashindwa kuelewa kwamba hicho ndo chanzo cha wanafunzi wengi kufeli

  5. Na je kama mwanafunzi alikuwa anapata sifuri tangu awali kwa nini wameufuta mtihani wa kidato cha pili ambao ulikuwa ni muhimu kwa ajili ya kumpima mtoto kabla ajavuka kwenda kidato cha tatu?

  6. Na bado tumeshuhudia kuboronga kwa wizara hii kwa kuweka maswali ya multiple choice ya hesabu kwa mtihani wa Darasa la saba waliomaliza hivi karibuni hapo tusitegemee kuboresha somo la hesabu kwani mtoto anaweza kuwa hajui hesabu lakini akabuni nakubahatisha akaongoza kitaifa.

  **Chanzo cha habari hii ni Tanzania Daima**
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyo waziri hafai hata kidogo. Shule yenye mwalimu mmoja wanategemea watoto wafundishwe na nani? Watoto wanakalia ndoo, watasomaje? Kapataje huo uwaziri kama anashindwa kuelewa tatizo lililopo kwenye idara yake?
   
 3. c

  choka Senior Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la viongozi wetu,hawana uzalendo,wala upendo kwa wananchi wanao waongoza,na kama wangeweza kuwa na uzalendo na upendo,wala leo hii tusinge zungumzia kufeli kwa wanafunzi,mimi naamini wanafunzi wanaweza kufanya vizuri,endapo vitu muhimu vingetekelezwa na viongozi wetu,mfano.
  Walimu wangepatiwa mishara mizuri.
  Maabara zingetengenezwa.
  Vitabu vingekuwepo vya kutosha.
  Chakula kwa wanafunzi,usafiri.na vinginevyo vingi tu.
  Hivi vingefanya wanafunzi wawe huru,na wangekuwa wanajua jukumu lao ni kusoma tu.
  Lakini kutokana na viongozi wetu,kupenda sana porojo,na kujali maslahi yao zaidi,basi watoto wa walala hoi wanatolewa kafara na kufeli.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..wanafunzi wa form 4 ni watoto hao siyo watu wazima.

  ..wanapofanya vibaya ktk masomo tunapaswa kuwahoji WAZAZI na WAALIMU.

  ..Waziri angeeleweka kama angekuwa anazungumzia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.
   
 5. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi bado nitaendelea kuwalaumu watanzania, waziri kama huyu ni wa kumchukulia hatua ajiuzulu hatufai. Huyu waziri yaelekea yuko ktk wadhifa wake kwa maslahi yake na ya waliomteua.
   
 6. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  mimi napenda niungane na mawazo ya mheshimiwa waziri moja kwa moja.kwanza siyo kweli kuwa shule hazina vitabu,vitabu vipo, walimu wapo kwa wasitani walimu 6 kila shule.tatizo kubwa lipo kwa wanafunzi wenyewe. hawajui kwanini wapo shule.tatizo la pili ni baadhi ya wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao.siku hizi wanafunzi wanapenda kufaulu bila kusoma,kitu ambacho hakiwezekani.mwanafunzi mwenye nia ya dhati ya kusoma lazima atafaulu.wanafunzi hawapendi kusoma vitabu,hawafiki shule,hawapendi mitihani,sasa hapo atafaulu vipi? maswali ya kuchagua ktk somo la hisabati siyo tatizo maana huwezi kujua jibu sahihi bila kukokotoa. TATIZO WATANZANI TUMEZIDI KUENDEKEZA SIASA,UKIAMBIWA UKWELI HUPENDI. mimi najua kwamba ukitaka kwenda mbinguni sharti ufe.Na ukitaka kufaulu sharti ukubali kujinyima starehe na uhangaike kuitafuta elimu kwa udi na uvumba.
   
 7. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  endelea kuwaza hivyo hivyo kijamaa bila kujali dunia inaelekea wapi. mimi naamini elimu ndio kila kitu ukitaka maendeleo ambatana na elimu. utabaki kumlaumu waziri mpaka lini?? siku hizi wanafunzi wanapenda starehe kupindukia. wanakunywa pombe kupindukia,wanapenda miziki ni kila aina ya starehe kupitiliza sasa elimu na mambo hayo wapi na wapi?? wanafunzi na familia ambazo wanafuatilia elimu vizuri wanafanya vizuri hata kama watasoma shule ya kata yenye walinmu 5.mbaazi akikosa maua husingizia uwa. SOCRATES ALISOMA KWENYE SHULE YA WALIMU WAWILI MBONA ALIKUWA GREAT THINKER!!!
   
 8. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mkuu nakupinga kwa nguvu zote! Kama mwanafunzi alifaulu darasa la Saba, kwenda shule za Kata then anapata Zero. Kuna tatizo somewhere. Kutukana wanafunzi peke yao ni kuwaonea, kulaumu walimu pia sio sahihi maana wamekuwa na migogoro na serikali years now. Wizara ya elimu kama whatchDog ndio ya kulaumiwa kwa kutelekeza wajibu wake. Lazima tukubali elimu iliosomeshwa 20yrs ago ni tufauti na elimu inayosomeshwa sasa. Kwa hiyo tusilinganishe wanafunzi wa sasa kwa vigezo vya enzi. Serikali lipa madeni ya walimu, serikali peleka qualified teacher vijijini na shule za kata.
   
 9. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Mkuu umeeleza mambo mazuri sana ila hapo kwenye red napingana na wewe, upande wa walimu kuna shule nyingi sana
  zina upungufu wa walimu hilo bado ni tatizo hasa huko vijijini maana walimu wengi wanataka wakae mjini, halafu hapo kwenye hesabu hilo ni tatizo kubwa sana maana aina hiyo ya maswali huchangia kudumuza kiwango cha utafiti wa mwanafunzi kwa sababu badala ya kukokotoa wengi wao hubuni majibu.Pamoja mkuu
   
 10. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mnajua jinsi alivyopewa huo uwaziri? Anakwepa ukweli uliomchungu! Shule za kata wanasoma watoto wa masikini, wa akina mulugo wanasoma shule nzuri ili kuandaliwa kuwa viongozi baadae!
   
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Manina zake..... We need his scores
   
 12. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  wewe uko nchi gani? Hujui kwamba watoto wanafaulu mtihani wa darasa la saba lakin hawajui kusoma na kuandika.Unategemea waendeleze wimbi la ushindi wakiwa hawajui kusoma na kuandika wakiwa sekondari? Haiwezekani
   
 13. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Je wanajifaulisha wenyewe au Mamlaka husika huwachagua kujiunga sekondari? Ni kosa la mwanafunzi au wanaomchagua? kwa hiyo si kosa la wanafunzi bali ni serikali
   
 14. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,160
  Likes Received: 1,162
  Trophy Points: 280
  Boss wake anaamini Wanafunzi anayepata mimba ni Uzembe wake!
   
 15. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kwenye Red naomba tu nipishane na wewe kimaono vitabu vinawza kuwepo lakini unajua kuleta vitabu pasipo mwanafunzi kujua kusoma ni mapambo. inabidi wa wepo walimu wa kuwafundisha kwanza ndio vitabu vipate dhamani. Swala la wastani wa walimu sijui kama unaelewa maana ya wastani na umejikita katika maana ipi kama wewe ni mtaalam wa hesabu za takwimu kunajia nyingi sana naomba nikupe mfano huu (2, 24, 5, 30, 1) ukitafuta wastani hapo utakuwa unanyanyapaa shule zingine ndio ilivyo kwa walimu wa tanzania mji walimu wengi na vijijini 1,2,3,4,5 hadi 6 unayosema. kufaulu bila kusoma hii haihitaji kama umesoma nyakati zetu hakukuwepo wimbi au utititli wa ufaulu kama huu nakumbuka ilikuwa hata nadra kwa mwanafunzi ndani ya kata kufaulu lakini leo hii yani kufauli ni kama pai sishangai kuona wanafunzi wanafaulu na kwenda sekondari wanafail. hili la wazazi nakubaliana maana watoto wengi wanakaa na mahoyse girl wazazi wengi wako busy na shughuli za kimaisha. ulishaona lini hesabu ikafanywa kwa kuchangua? hapa tutegemee taifa lisilojua hesabu maana wengi watakuwa wanapita kwa kuibia maana ni rahisi kuibia kama ni herufi inaweza tumika hata ishara na mtu kufaulu lakini kwa kukokotoa haiwezekani kuibia otherwise amepatiwa njia
   
 16. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  The way unaongea ni km vile huna taaluma ya education lakini unafahamu vitu partially. Mimi ni Educationist na ninajua hilo eneo vema sana. Km kuna wanafunzi wanapenda kufeli basi ni 5% tu wengine wote wanatengenezewa mazingira ya kufeli. Shule na wastani wa walimu 6 kwa minimum ya wanafunzi 400 kila shule ni uwiano wa mwl mmoja kwa wanafunzi 66. Hakuna elimu hapo. Hivi sasa Britain uwiano wa mwl kwa mwanafunzi ni 1:5, unajua unachokisema kweli?
   
 17. B

  Benito Josh Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Tatizo linaanzia kwa mwanafunzi mwenyew then wazaz then serikari then walimu.
   
 18. bologna

  bologna JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 1,155
  Likes Received: 908
  Trophy Points: 280
  Sio kila kitu mnalaumu tu wana JF. Wanafunzi wanazingua sana mashuleni, wachache sana wanaokaza wengi wanaendekeza usela usiokua na tija. Wasichana ndio usiseme full kujiachia kama watu wazima. Sisi tumesoma kitambo tena bila hata hao waalimu na still tumetoka. Hayupo mtu wakuleta vidonge vya kukufanya ufaulu, hapo ni msuli wako tu darasani. Mashule meeeeeeeeeeeeeeengi then yamejaa vilaza tu. MWANAFUNZI HANA MALENGO, MZAZI HANA MIPANGO, UNATEGEMEA MWALIMU ATAFANYA NINI HAPO. Watoto wadogo wanakanda NGANO badala kuingia darasani, leo hii unategemea nini.
   
 19. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  mimi nimefundisha darasani miaka 20,katika shule nilizopita wanafunzi walikuwa wanajua nini wamefuata shule na ndio maana hata kazi yangu haikuwa ngumu wanafunzi unawaelekeza kidogo wanakwenda kujiongezea maarifa vitabuni na group discussions. siku hizi mambo ni tofauti. nimewahi kukaa shule moja hata ukiacha popote kitabu kizuri utakikuta salama hakuna wa kuiba au hata kusoma.mvua ikinyesha kidogo tu tegemea zaidi ya nusu hawatafika shule.hata mwalimu akiwaita warudi awafundishe bure baada ya vipindi hawaendi.sasa hapo utailaumu serikali???? mimi ni mwalimu wa maths,kwenye mtihani wanafunzi wanasimamiwa ipasavyo kwahiyo hata mtihani ukiwa wa kuchagua ni lazima mwanafunzi akokotoe kwanza ndio apate jibu.in shot,tatizo la msingi lipo kwa wanafunzi then wazazi na pengine kidogo kwa serikali.:director:
   
 20. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  mimi ni educationist tena wa kitambo my swahili and good English can explain better.back to the point,wanafunzi wa siku hizi starehe,ujuaji,na pengine mazingira wanayotoka siyo rafiki wa elimu.hawapendi kusoma.huwezi kufaulu bila kujituma na kuitafuta elimu kwa udi na uvumba.katika baadhi ya shule notably pwani,lindi,na mtwara mwalimu kila siku anafundisha wanafunzi wapya.mwanafunzi aliye kuja jana kesho haji kwa hiyo mwalimu anaendelea kufundisha mada kumbe wanafunzi ni wapya!!! NO CONTINUITY NO UNDERSTANDING. Hapo tatizo ni la mwanafunzi hafiki shule.aliye anda mazingira ya kufeli ni mwanafunzi mwenyewe.HE WHO THINKS EDUCATION IS EXPENSIVE LET HIM OR HER TRY IGNORANCE.Wanaopenda shule hata huko kwenye shule za kata watapeta tu.
   
Loading...