Wanafunzi wamjeruhi mwanaume (53) sehemu za siri

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
852bcbcaad41048c52df20054cf6b539

Moshi. Mwanamume mmoja, mkazi wa Lole Marera, mwenye umri wa miaka 53, amejeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika korodani moja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea saa nne usiku Machi 7 katika eneo la Marera, Moshi.

Alisema vijana wawili; wa kiume (18) na wa kike (14), wanashikiliwa na polisi wakihumiwa kuhusika na tukio hilo.
“Mtu huyu alijeruhiwa akiwa nyumbani kwake na vijana hao ambao ni wanafunzi na majina yao yanahifadhiwa. Majeruhi amelazwa Hospitali ya Kilema akiendelea na matibabu,” alisema Issah na kuongeza kuwa watuhumiwa ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lyakrimu.
“Bado hatujajua chanzo cha tukio hili, au kulikuwa na nini kati ya mtu mzima huyo na hao wanafunzi kiasi cha kufikia hatua ya kujeruhiwa sehemu hizo hatari.”
Kamanda Issah alisema, “Lakini shauri hili likifika mahakamani inaweza kujulikana nini ambacho kilijiri na haki ikatendeka kwa baba huyo na hata wanafunzi.”
Jaston Msenga, mdogo wa majeruhi huyo aliliambia Mwananchi kuwa siku ya tukio kaka yake alitoka kazini na akiwa njiani alikutana na vijana waliomvamia na kumpiga kwa kitu kizito, kisha kumchana na kitu chenye ncha kali baada ya kuanguka.
“Baada ya kutoka kazini saa 2:30 usiku alipita mahali akanywa soda, na huwa anahifadhi fedha zake kwenye bukta. Sasa alipokuwa anatoa inasemekana wale vijana walimuona na alipoondoka ndipo walimfuata na kumpiga kisha kumchana (sehemu za siri) na walichukua fedha zake Sh300,000 ambazo zilikuwa za mafundi, ila kuna kijana mmoja bado anatafutwa,” alisema.
 
Pesa zote hizo kwanini asichukue ulinzi (escort ) wa polisi kama sheria inavyotaka?
 
Hahahahaaa! Ulinzi kwa mia tatu elfu?Je askari wangemtamani nao?
Nimeona comment yako. Ikibidi nirudi mwanzo mwa Mada nijue alikuwa na milioni 300,au Laki 300,nikajikuta naishiwa pose
Hizo ni hela za madafu unaongelea chini ya dola 130 za kimarekani. Hela ya kununulia viatu vya kawaida!

Kiasi kikubwa ni kuanzia shilingi ngapi na katika mazingira gani?
 
Mchagga kwa PESA!!!!Halafu tunataka kuaminiwa? Si mtoto si Mkubwa ni hatare cccc Ufoooo SARRO
 
Back
Top Bottom