Wanafunzi WakiTanzania Russia-Msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi WakiTanzania Russia-Msaada

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by VUVUZELA, Jun 27, 2011.

 1. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  WANAFUNZI WA KITANZANIA - CHUO KIKUU CHA URAFIKI LUMUMBA, MOSCOW-URUSI.

  Mhe. Waziri Mkuu Peter Mizengo Pinda,

  Tunaomba kuanza kwa kukupa pole kwa majukumu mazito uliyo nayo katika ujenzi wa taifa letu. Pia tunakupongeza kwa uimara na ushupavu wako katika kusimamia masuala mbalimbali ya kimaendeleo nchini.
  Mhe. Waziri Mkuu,sisi wanafunzi wa kitanzania katika Chuo Kikuu Cha Urafiki – Lumumba kilichopo jijini Moscow inchini Urusi tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kuweza kutupatia udhamini wa masomo ya elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Kwani fursa hiyo ni moja ya njia za kuelimisha taifa na pia kuongeza idadi ya watendaji bora katika sekta mbalimbali nchini.
  Mhe. Waziri Mkuu, lengo kuu la waraka huu kwako ni kukufikishia malalamiko yetu moja kwa moja juu ya kero mbalimbali tunazozipata kuhusiana na zoezi zima la mikopo hii tunayopatiwa na serikali yetu. Tumeamua kufikisha malalamiko haya kwako kwa sababu wahusika wakuu (WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI pamoja na BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU) hawataki kusikiliza kilio chetu. Tumeawaandikia barua nyingi sana kuhusiana na malalamiko yetu pasipo kujibiwa jibu lolote, na sisi hatuwezi kuendelea kukaa kimya huku tukizidi kuumia, wakati serikali ina kila sababu ya kutusikiliza kwani hii ni haki yetu ya msingi kabisa.
  Mhe. Waziri Mkuu, malalamiko yetu ni haya yafuatayo:
  1:UTARATIBU MBOVU WA MALIPO YA FEDHA ZA ADA.
  Kila mwaka bodi imekuwa na utaratibu wa kutokulipa ada kamili za wanafunzi kwa wakati. Baadhi ya wanafunzi hufikia hatua ya kutoa fedha zao za kijikimu ili kufidia mapungufu hayo katika malipo ya ada.
  Mfano:
  Mwaka 2008/2009 baadhi ya wanafunzi walilazimika kulipa sehemu ya ada toka katika fedha zao za kujikimu. Na pia mpaka leo haijulikani sehemu ile ya ada za wanafunzi hao ilikwenda wapi licha ya kuuliza mara kwa mara juu ya suala hilo Wizarani na Bodi kwenyewe.
  Mwaka huu 2010/2011, bodi imechelewa kutulipia ada kwa takrirban miezi 9 (kwani ada ilitakuwa kulipwa mwezi wa 9 mwaka jana(2010) lakini imekuja kulipwa mwaka huu wa 2011 mwezi wa 5, wakati ndiyo mhula wa pili unaisha. Na cha kusikitisha zaidi wanafunzi walio wengi wamelipiwa ada pungufu kwa zaidi ya dola 1000 kwa kila mwanafunzi, na wengine hawakulipiwa kabisa.
  Mhe. Waziri Mkuu, hii ni kero kubwa sana kwani mara kwa mara tumekuwa tukifukuzwa madarasani kwa sababu hatujalipa ada. Tunadharirika sana. Na hata sasa baadhi yetu wametangaziwa kutokufanya mitihani yao ya kuhitimu shahada ya kwanza(degree) na wengine mitihani yao ya kufunga mwaka. Na hali hii hutokea kila mwaka.
  2:MAKATO KATIKA FEDHA ZA KUJIKIMU
  Mhe. Waziri Mkuu, tunasikitika sana kusema kuwa ni jambo lililozoeleka sasa kwa Bodi kutukata fedha zetu za kujikimu kila mwaka . na kila mara tunapodai kiasi kilichokatwa, wamekuwa wakisema fedha zinapungua kwa sababu ya rate of exchange pale wanapobadili fedha za kitanzania (shilingi) kwenda dola za kimarekani (USD), lakini cha ajabu ni kwamba wakati mwingine ada inapopungua bodi huwa inafidia kiasi kilichopungua. Je, ina maana fedha zetu za kujikimu tu ndizo zinazostahili kuathiriwa na rate of exchange na kutokufidiwa kiasi kinachopelea kila mwaka?
  Mfano mzuri ni mwaka huu wa 2010/2011. Bodi imetuma kwa kila mwanafunzi fedha pungufu za kujikimu kwa wastani wa dola za kimarekani 477 na bado wakatueleza eti ni kwa sababu ya rate of exchange. Tumewaomba sana watutumie fedha hizo kwani sisi tunaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na makato hayo, lakini mpaka leo hatujapatiwa jibu lolote wala hatuoni dalili zozote za suala letu hilo kushughulikiwa na Bodi ya mikopo wala Wizara ya elimu.
  3:KUTOKUTUMIWA FEDHA ZA BIMA YA AFYA .
  Mhe. Waziri Mkuu, mwaka huu wa 2010/2011, serikali haikutupatia kabisa fedha za kulipia bima ya afya. Kwa masharti ya chuoni na Nchini urusi, mwanafunzi kama HUJALIPIA BIMA YA AFYA HUWEZI KUPATIWA HUDUMA YOYOTE ILE YA AFYA, HUWEZI KURUHUSIWA KUFANYA USAJILI WALA KUPATWA VIZA(kila mwaka huwa tunahitajika kuomba viza mpya na kufanya usajili ili tuweze kuruhusiwa kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuata). Licha ya kuikumbusha wizara na bodi juu ya kutupatia fedha hizo, lakini mpaka leo mwaka unaelekea kuisha hatujapatiwa fedha hizo wala hakuna jibu la aina yoyote ile.
  4:MWAMBATA WA ELIMU.
  Mhe. Waziri Mkuu, ni miaka mingi sasa imepita tangu tuanze kuiomba wizara kutuletea mwambata wa elimu nchini urusi. Matatizo yetu mengi yanachelewa sana kupatiwa ufumbuzi na wakati mwingine yanashindikana kabisa kupatiwa ufumbuzi kwa sababu hatuna mwambata wa elimu nchini urusi. Mara kwa mara tumelazimika kupeleka matatizo yetu kwa maofisa wa ubalozi ambao nao pia wana majukumu yao mengine tofauti tofauti, tunashukuru wamekuwa wakijitahidi kutusaidia. Lakini kukosekana kwa Mwambata wa elimu bado ni tatizo kubwa sana linalotuathiri wanafunzi nchini urusi.
  5: OMBI LA NYONGEZA KATIKA FEDHA ZA KUJIKIMU.
  Mhe. Waziri Mkuu, mara kwa mara tumekuwa tukiilalamikia na kuiomba Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi kutupatia nyongeza ya fedha za kujikimu pasipo mafanikio yoyote. Mji tunaoishi (MOSCOW) ni mojawapo ya miji ghali sana duniani, maisha yetu huku yameendelea kuwa duni sana na wakati mwingine tunashindwa hata kupata baadhi ya huduma muhimu. Mara kwa mara tumeijulisha wizara ya elimu, na hata tumeweza kuipatia michanganuo inayoonesha jinsi fedha wanazotupatia kwa sasa zinaishia katika kulipia mambo mbalimbali ya lazima na wakati mwingine tunabakiwa na kiasi kidogo sana cha pesa ambacho ndicho tunalazimika kukitumia kwaajili ya chakula(japokuwa wengi wetu tunakula aidha mlo moja au miwili tu kwa siku). Kwa kweli tunaiomba serikali kutufikiria katika jambo hili kwani hali tuliyonayo kwa sasa ni mbaya sana, pia ikizingatiwa kuwa nchini Urusi KILA MWAKA MWEZI WA 9 BEI ZA BIDHAA NA GHARAMA ZA HUDUMA MBALIMBALI HUPANDISHWA na hivyo kuzidi kutuathiri zaidi sisi wanafunzi wa kigeni.
  Mhe. Waziri Mkuu, tunatumaini kuwa malalamiko, vilio na maombi yetu, utayapokea na kuyafanyia kazi mapema. Tunakutakia afya tele na mafanikio mema katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa letu.
  Asante sana.
   
 2. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jamani ndugu zetu wanaomba msaada!!
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Khaaah!si bora kubaki bongo tu...poleni sana wakuu.
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  no kuna umuhimu wa kusoma nje mkuu sema tu serikali ya sasa sio sikivu hasa kwa elimu ya juu!!pia na ninyi wanafunzi jitahidini sana mara mpatapo boom mjibane hali ya uchumi kwa tanzania ya sasa sio nzuri ni ufisadi tu mwingi wabunge wanajipendelea yaani naamini itafika wakati serikali inaweza kufuta hata scholarships za nje viongozi wetu wamekua vilaza sana!
   
 5. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tafuteni namna ya kugoma au kufanya maandamano. thats the only way to get your rights from Tanzanian Govt. Waulizeni wenzenu bongo hapa kama walishafanikiwaga bila mgomo au maandamano.
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  sasa kama wa2 wanateseka hvo mkuu,c bora m2 ubaki 2 home ulie msoto kwenu kuliko kutesekea kwenye nchi ya wa2,tena russia!hii serikali bana,sasa iliwapeleka wa nin huko ka ilijua itashndwa kuwagharamia?
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Russia kunani mkuu?
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  russia ni moja ya mataifa ambayo maisha yake ni ghali sana hapa duniani.
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  .......sijaona sehemu ghali kama kule....box lenyewe hakuna baridi mpaka makende yanaganda.......hakuna XXXL ya kuoa u survive.....hawa watoto watauza tigo wallahi wasiposaidiwa
   
 10. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo umekwenda mbali sana na utakuwa umewadhalilisha vijana hawa. Haifai namna hiyo. Tuangallie jinsi gani ya wao kusaidiwa na sio kuwakejeli
   
 11. SAWEBOY

  SAWEBOY JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Hivi kuna sababu gani wewe kwenda kusoma First degree huko Russia? mbona shida zingine mnajitafutia nyie watoto? enheee maana mkishasikia kupanda pipa basi mnakuwa kama wehu fulani hivi, na mnaona kama ndo mmeshamaliza hii dunia yoote! kumma bruku zenu! sasa huko cha moto lazima mkione coz ya uendawazimu wenu pamoja na wazazi wenu.

  Kinachosikitisha ni kuwa watoto wengi wanaolipiwa na bodi ya mikopo kusoma undergraduate degree nje ni mitoto ya vigogo ambao ni mafisadi serikalini, na ukiona perfomance zao ni za ukilaza kabisa but still bodi ya mikopo inawalipia huko nje! mnanikera sana shezi zenu!

  Sasa mtajiju sisi na qualification zetu tunakamua skonga huku nje bila shida kula kuku kwa kwenda mbele, ada + money allowance hata zinakotafutwa sisi hatujui but tunaponda raha tu, first degreee UDSM as usual, nyie lieni tu huko manyau nyie!! walilieni baba zenu mafisadi waliofight hizo chance kwa kutaka kuwaumiza watz!

  Kuna sababu gani wewe ukasomee bachelor huko Russia wakati wewe ni kilaza tu? shame on you!
   
 12. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Maneno mazito sana mkuu. Sawa najua kuna watoto wa vigogo lakini pia ikumbukwe wapo wale watoto wa walala hoi pia
   
 13. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  sidhani kama wewe ni mtanzania mkuu!
   
 14. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati mbaya sana kuna Watanzania wasiojua namna nzuri ya kujieleza . Kichwa cha habari ni msaada sasa si vizuri kutoa maneno makali , hapa si mahali pake,zaidi ya hayo hakuna anayelazimishwa kuchangia. Kumbuka kuandika matusi ni kupoteza muda na kujitafutia laana. Poleni sana ndugu zetu huko URUSI sisi huku Cuba tupo pamoja na nyie,,,WE SHALL FIGHT FOR RIGTHOUSNESS. GOD MAY HELP US.
   
 15. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Poleni sana mkuu I hope mtoto wa mkulima atawasikia kilio chenu, msiache kudai haki zenu
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  aaaggh! Sijui kwanini nimelisoma hili lipost.Kuwa na huruma japo kidogo, watu wanalia shida we unawaongezea maumivu. hao madogo wakati wanaenda huko walikuwa wanajua mkataba wao na HESLB upo vipi ila bodi ndio inawaangusha.Hayo yote maisha, maisha popote.
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Imagine madent wa nyumbani kila siku hela hadi kwa migomo sasa huko Russia ndio watalazwa na njaa ama kuishia kuwa homeless. Poleni sana, najua mnateseka ukizingatia kuna hao Russian skinheads wanaowawinda na kuwapiga na kuwaua wageni hasa blacks
   
 18. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #18
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Dahhhh
  Poleeni sana kwa kweli...
   
 19. g

  gracious86 JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 433
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kuwa na roho ya huruma bas japo kidogo! Duuuh! Hopefully wewe si mtanzania
   
 20. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Mmmmnnhhh
   
Loading...