Ilikuwa Jumatatu tarehe 2 Agost 2021,kwenye maeneo ninayoishi, nilikutana na wanafunzi wengi wakirejea nyumbani. Sikujishughulisha kujua tatizo.
Naenda mbele zaidi nilikuta mjadala kwamba wanarudi hawataki kuchanjwa dhidi ya covid19. Mzazi mmoja akapiga simu kwa mwalimu, akajibiwa hakuna chanjo shuleni wala taarifa ya kuwepo kwa chanjo. Mwalimu ameshangaa kuona watoto madarasani wako pungufu.