Wanafunzi wa UDOM waliosimamishwa masomo, Wizara ya Elimu ni lini mtatoa kauli juu ya hili?

phillipinne

New Member
Jun 27, 2016
4
7
Ni mda sasa tangu wanafunzi wa stashahada maalumu ya ualimu wa hisabati, Sayansi na TEHAMA katika chuo kikuu cha Dodoma kuahilishiwa masoma baada ya serikali kuamua wanafunzi hao kurudishwa nyumbani kwasababu ambazo kila kiongozi wa serlikali alizijua yeye mwenyewe lakini mwisho wa siku sababu iliyosikika ni tatizo la ufaulu.

Taarifa kupitia wizara ya elimu ilisema watapitia kiwango cha ufaulu wa wanafunzi hao kwa haraka na kutoa majibu ambayo yatajibu hatima ya wanafunzi wale. Jambo la kushangaza mpaka sasa hakuna taarifa yoyote juu ya hili wala hakuna kauli yoyote toka serikalini kuhusu hatua iliyofikiwa juu ya wanafunzi hao.Ikumbukwe wengi ya wanafunzi wale ni watoto wadogo wanaotokea familia maskini hasa vijijini.

Mbaya jambo hili mwanzoni liliibua hisia kali sana ila baadae limekosa hata mtu wa kulifatilia ili watoto hawa wawe na taarifa juu ya hatua na namna jambo hili linashughulikiwa.Ni vizuri mtu kuwa na taarifa sahihi ili kufanya mamuzi sahihi, hivyo basi wanafunzi wale wanahitaji taarifa sahihi kuliko fununu ili waweze kuamua kwa usahihi pia.

Si vizuri kuendesha nchi kwa matukio kwani hii itafanya mambo mengi kuwa kama yamesahaulika au yametatuliwa kumbe bado.Mimi nadhani imefika wakati serikali itoe mwendelezo wa jambo hili la wanafunzi wa UDOM ili na wao wawe huru kuliko kwendelea kusubiri kitu wasichokijua katika mazingira ya giza. Waziri wa elimu tujuze mmefikia wapi katika swali hili kumbuka mwanzoni ilisema itachukua mda mfupi kama wiki mbili Mh waziri wa elimu.
 
Mmmh siasa bhana,,,, ndo maana sijawah kua mfatiliaji wa siasa,,,, Kuna Watu walienda adi stand kukaa nao,,, Au ndo natafuta kik,,,, Daaaaaaa mi Napita tuuuu,,,, tuliona hili tukio inauma sana Eti,,,,,
 
Back
Top Bottom