BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Posted Date::10/3/2007
Wanafunzi Muhimbili watangaza mgomo wadai hawana pa kuishi
Na Andrew Msechu
Mwananchi
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili wametangaza mgomo usio na ukomo mpaka uongozi wa chuo hicho utakapotelekeza madai ya kupatiwa mahali pa kuishi .
Madai ya wanafunzi hayo ni kukabidhiwa rasmi hosteli za chuo hicho zilizopo mtaa wa Chole jijini Dar es Salaam, kwa madai kwamba hawana mahali maalum pa kuishi , huku baadhi ya nyumba za wageni jijini.
Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi mgomo huo kwa wanafunzi wa chuo hicho, Rais wa Serikali ya Wanafunzi (Muhasso), Edwin Chitage alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutofikia makubaliano baina ya uongozi wa wanafunzi na ule wa chuo juu ya hatima ya hosteli hizo.
Alisema kuwa hosteli hizo zilitakiwa kukabidhiwa kwa uongozi wa chuo miaka sita iliyopita na kutakiwa kufanyiwa matengenezo baada ya serikali kukubali kutoa Sh1.2 bilioni, lakini mpaka sasa wanafunzi wameshindwa kuingia.
?Tunashangaa uamuzi wa uongozi wa chuo kutotilia maanani suala hili, tumejaribu kufanya kila juhudi, lakini hakuna mafanikio, angalia, kwa mwaka wa kwanza tu wenye wanafunzi wapatao 310 ni wanafunzi 124 tu ndiyo walioweza kupata hosteli, wengine wamekuwa wakiishi maeneo ya hatari kwa kupanga vyamba huko Magomeni na Manzese na hakuna anayetaka hata kujua wanaishije,? alisema na kuongeza
?? haya yote yanatokea wakati hizi hosteli za Chole zenye uwezo wa kuchukua watu 640 zikiwa zimekamilika, lakini kinachotushangaza zaidi ni taarifa za uongozi wa chuo kutafuta mwekezaji ili kuziendesha, hatuafikiani kabisa na suala hilo?.
Makamu wa Rais wa Serikali hiyo, Mmoto Mahadhi, alidai kuwa dhana hiyo inatokana na hali halisi iliyopo, watoto wa matajiri na viongozi wakiishi kwenye hosteli za gharama kubwa zilizopewa jina na Richmond, huku watoto wa maskini wakiishi kwenye hostel nafuu maarufu kwa jina la Darfur.
?Huko Richmond ndipo wanapoishi watoto wa wakubwa serikalini ambao wana uwezo wa kulipa gharama aghali zinazofikia Sh1.8 hadi 2.4 milioni kwa mwezi, wanaoumia ni sisi watoto wa hohehahe, tupewe hosteli hizo tupunguze adha ya wanafunzi kuteseka,? alisema.
Akizungumzia suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Kisari Pallangyo, alisema tatizo la hosteli kwa chuo hicho linatokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi linalotokana hitaji kubwa la watumishi wa sekta ya afya kwa sasa, hivyo chuo kuongeza wanafunzi wanaodahili.
Hata hivyo, alisema malalamiko ya wanafunzi kwa sasa hayana msingi kwasababu tayari chuo hicho kilishawaeleza kupitia barua za kujiunga chuoni hapo kuwa hakina uwezo wa kuwapatia hosteli za kuishi.