Wanafunzi Muhimbili watangaza mgomo wadai hawana pa kuishi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Posted Date::10/3/2007
Wanafunzi Muhimbili watangaza mgomo wadai hawana pa kuishi
Na Andrew Msechu
Mwananchi

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili wametangaza mgomo usio na ukomo mpaka uongozi wa chuo hicho utakapotelekeza madai ya kupatiwa mahali pa kuishi .

Madai ya wanafunzi hayo ni kukabidhiwa rasmi hosteli za chuo hicho zilizopo mtaa wa Chole jijini Dar es Salaam, kwa madai kwamba hawana mahali maalum pa kuishi , huku baadhi ya nyumba za wageni jijini.

Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi mgomo huo kwa wanafunzi wa chuo hicho, Rais wa Serikali ya Wanafunzi (Muhasso), Edwin Chitage alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutofikia makubaliano baina ya uongozi wa wanafunzi na ule wa chuo juu ya hatima ya hosteli hizo.

Alisema kuwa hosteli hizo zilitakiwa kukabidhiwa kwa uongozi wa chuo miaka sita iliyopita na kutakiwa kufanyiwa matengenezo baada ya serikali kukubali kutoa Sh1.2 bilioni, lakini mpaka sasa wanafunzi wameshindwa kuingia.

?Tunashangaa uamuzi wa uongozi wa chuo kutotilia maanani suala hili, tumejaribu kufanya kila juhudi, lakini hakuna mafanikio, angalia, kwa mwaka wa kwanza tu wenye wanafunzi wapatao 310 ni wanafunzi 124 tu ndiyo walioweza kupata hosteli, wengine wamekuwa wakiishi maeneo ya hatari kwa kupanga vyamba huko Magomeni na Manzese na hakuna anayetaka hata kujua wanaishije,? alisema na kuongeza

?? haya yote yanatokea wakati hizi hosteli za Chole zenye uwezo wa kuchukua watu 640 zikiwa zimekamilika, lakini kinachotushangaza zaidi ni taarifa za uongozi wa chuo kutafuta mwekezaji ili kuziendesha, hatuafikiani kabisa na suala hilo?.

Makamu wa Rais wa Serikali hiyo, Mmoto Mahadhi, alidai kuwa dhana hiyo inatokana na hali halisi iliyopo, watoto wa matajiri na viongozi wakiishi kwenye hosteli za gharama kubwa zilizopewa jina na Richmond, huku watoto wa maskini wakiishi kwenye hostel nafuu maarufu kwa jina la Darfur.

?Huko Richmond ndipo wanapoishi watoto wa wakubwa serikalini ambao wana uwezo wa kulipa gharama aghali zinazofikia Sh1.8 hadi 2.4 milioni kwa mwezi, wanaoumia ni sisi watoto wa hohehahe, tupewe hosteli hizo tupunguze adha ya wanafunzi kuteseka,? alisema.

Akizungumzia suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Kisari Pallangyo, alisema tatizo la hosteli kwa chuo hicho linatokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi linalotokana hitaji kubwa la watumishi wa sekta ya afya kwa sasa, hivyo chuo kuongeza wanafunzi wanaodahili.

Hata hivyo, alisema malalamiko ya wanafunzi kwa sasa hayana msingi kwasababu tayari chuo hicho kilishawaeleza kupitia barua za kujiunga chuoni hapo kuwa hakina uwezo wa kuwapatia hosteli za kuishi.
 
Makamu wa Rais wa Serikali hiyo, Mmoto Mahadhi, alidai kuwa dhana hiyo inatokana na hali halisi iliyopo, watoto wa matajiri na viongozi wakiishi kwenye hosteli za gharama kubwa zilizopewa jina na Richmond, huku watoto wa maskini wakiishi kwenye hostel nafuu maarufu kwa jina la Darfur.

?Huko Richmond ndipo wanapoishi watoto wa wakubwa serikalini ambao wana uwezo wa kulipa gharama aghali zinazofikia Sh1.8 hadi 2.4 milioni kwa mwezi, wanaoumia ni sisi watoto wa hohehahe, tupewe hosteli hizo tupunguze adha ya wanafunzi kuteseka,? alisema..

yani 2.4 million per month!!thats basically near 2000 usd!!per one year that clocks at arnd 24,000 usd!!damn 20 g'z for a hostel in dar???MUCHS??thats basically almost as good as what someone should pay for accomodation in Ivy league...,no disrespect but thats just over-rated.

no wonder twin towers costed so much..,wakubwa wetu serikalini have such a talent with numbers!!!

rushwa hizi..,2 much sasa..,

Akizungumzia suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Kisari Pallangyo, alisema tatizo la hosteli kwa chuo hicho linatokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi linalotokana hitaji kubwa la watumishi wa sekta ya afya kwa sasa, hivyo chuo kuongeza wanafunzi wanaodahili.

Hata hivyo, alisema malalamiko ya wanafunzi kwa sasa hayana msingi kwasababu tayari chuo hicho kilishawaeleza kupitia barua za kujiunga chuoni hapo kuwa hakina uwezo wa kuwapatia hosteli za kuishi.


as usual..,out of touch...,out of point...,pointless..,hakujibu alichoulizwa huyu nae..,

prof vipi hapa??au ndio uzee??


kuwa na univ bila accomodation arrangements ni uzembe tu..,no wonder hao jamaa wakitoka huko waumiao ni wagonjwa..,
 
Ifuatayo ni tahiriri ya mhariri wa gazeti la HabariLeo kuhusiana na sakata la wanafunzi chuo cha Muhimbili:

Muhimbili rejeeni madarasani, mgomo wenu umepitwa na wakati

Mhariri
HabariLeo; Friday,October 05, 2007 @00:01

WANAFUNZI wa kozi za chini katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba cha Muhimbili (MUHAS), jana walianza mgomo wa kutoingia madarasani ikiwa njia ya kuubana uongozi wa chuo wa kuwaruhusu kutumia hosteli za Masaki ili kupunguza tatizo la malazi linalowakabili.

Wanafunzi hao waligoma licha ya agizo la uongozi huo la kuwataka wasifanye hivyo vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Kama alivyosema Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Kisali Pallangyo, madai ya wanafunzi hao kuhamia hosteli za Masaki, hayana msingi kwa kuwa walikwishataarifiwa kwamba hazijakamilika.

Tunafahamu kwamba licha ya kuelezwa hivyo wanafunzi wakiongozwa na Serikali yao wanaendelea kung’ang’ania kwamba uongozi wa chuo umekataa kuwaruhusu kuhamia kwenye hosteli hizo kwa madai kuwa uongozi wa chuo unataka kumpa mwendeshaji binafsi ambaye hawamtaki kwa hofu kuwa atawatoza gharama kubwa ambazo hawataweza kuzilipa.

Kwa upande wake uongozi umejibu tuhuma hizo kwa kusema mgomo ulioanza jana hauwezi kamwe kupunguza tatizo la uhaba wa hosteli ambalo linakikabili Chuo Kikuu cha Muhimbili na vingine vya umma na vya watu binafsi.


Sote tunafahamu kwamba uhaba huo wa hosteli umejitokeza dhahiri mwaka huu kutokana na kuongezeka ghafla kwa idadi ya wanafunzi waliojiunga na vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na kupandishwa hadhi kwa baadhi ya vyuo hivyo, kikiwamo cha Muhimbili.

Laiti ungefikiwa uamuzi wa kutoongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu, baadhi ya hao wanaogoma kwa kucheleweshwa kwenda Masaki wangepata nafasi ya kuwa wanafunzi wa Muhimbili?

Ni kwa sababu hiyo tunawasihi wanafunzi waliogoma waone busara na mantiki ya uongozi wa chuo chao na warudi madarasani mara moja. Wasijaribu kupenyeza sababu za kisiasa na nyinginezo kulazimisha kuingia kwenye majengo ambayo hayana vitanda, magodoro, mghahawa, uzio, zahanati na meza za kusomea hazipo.

Maadamu wamehakikishiwa kwamba hosteli zitakamilika na watahamia huko, kinachotakiwa kutoka kwao ni subira.

Inafaa wanafunzi kukumbuka kwamba zama za kufanya migomo inayoweza kuhatarisha nafasi zao za kitaaluma chuoni zimepitwa na wakati kwani si tu zinaweza kuwasababishia kupoteza nafasi za kuingia tena darasani, bali hata kuishi kwenye hosteli za Masaki wanazolilia kuhamia sasa kwa udi na uvumba.

Source link: HabariLeo.

Je, huu mgomo umepitwa na wakati? Mgomo wa aina ipi huwa ndani ya wakati?..

SteveD.
 
Binafsi nimepitia UDSM, na situation ya Hosteli naijua...wakati mwingine huwa nafikiria nini kifanyike. Kugoma si suluhisho kwa sasa kwani tatizo nnaloliona tayari lipo serikali kuu juu ya Miundo Mbinu yake. Ikiwa nyumba za TTCL pale Boma kapewa MKUBWA afungue Hosteli zingefaa kwajili ya vijana wa MUCH kuliko kuwaweka mabibo. Najua kama PM anaweka mkazo juu ya primary education, hashindwi kufanya Harambee au Kutafuta hao serious investor wakajenga Hosteli within 1 year vijana wenzetu wakapata sehm nzuri ya kusoma...nashauri tutafute namna ingine ya kupata suluhisho lkn si kugoma
 
yaani hili movie limeanza tenaaa...hivi li serikali letu lina nini???haliishi kulalamikiwa?yah no one is perfect we agree lakini this is too much bwana..hao ndo wasomi wa sasa taifa la kesho if u dont create good mazingira ya kusoma for them now ni nani atakayekuja ongoza nchi bidae???au ndo wakubwa wanataka hiyo mitoto yao ambayo ni choka mbaya lakini imepelekwa nje kusoma ndiyo ije iwarithi wazazi wao??
na wewe usemaye migomo imepitwa na wakati waendelee na masomo...halafu wakitoka chuoni waje kulala kwako??majibu mengine tusiwe washabiki tuu wa serikali jamani..
ingawaje at the end kama kawa.kuna watakao surfer the coincidences...hapo tu ndio mie nahofia...as ni kawaida ukipigana na ukuta waumia mwenyeeweeeee
 
Aaah! Hili mbona simple tu? Si wapewe hostel kule Mlongazila campus, wawekewe na school bus la kuwachukua?
Haya mambo mengine yameshapatiwa ufumbuzi ni bureaucracy tu ndio inayozaa migomo kama hii....
MLONGA+PICHA.jpg

Kuna vyumba vyao huku vinakaliwa na popo...
 
Back
Top Bottom