Wanafunzi kupimwa kubaini waliokeketwa

LAMBOFGOD

JF-Expert Member
Aug 12, 2016
1,561
1,317
C:\Users\KAROLI\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.png

upload_2017-1-10_19-32-24.png

Hodi wanajamvi, Nimatumaini yangu yakwamba muwazima wa afya!!!!

Nina maswali machache juu ya mpango mkakati huu ambao uko mbioni kuwa implemented

1. Ni kifaa gani kitakacho tumika wakati wa kuwapima wanafunzi na human assistance itakayohusika itakuaje?

2. Kitendo cha kuwapima wanafunzi bila ridhaa yao kikoje hapa?

3. Side effect zitakaowapata waliokeketwa na wasiokeketwa limeangaliwaje hapo?

4. Je swala la kupima ndio njia pekee ya kumaliza tatizo la kukeketa watoto wa kike?

5. Kwa nini campaign isifanyike mikoa husika kuelimisha jamii kuliko kulenga watoto wa kike wasiokuwa na sauti kwa wazazi wao pindi maamuzi yaolewapo, wakati mikoa husika inajulikana bayana hapa nchini?

Nawasilisha karibuni kwa maoni yenu wanajamvi
 
Nimeisikia hii asubuhi radio free akili yangu ikabidi niiache kwenye friji.huo mkakati utaacha severe psychological trauma kwa mabinti zetu na sijajua baada ya hapo what next na nini faida yake.Ushauri kwa muheshimiwa apambane na kuweka juhudi kubwa kwenye kuzuia ukeketaji kuliko kupeleka juhudi kubwa kwenye zoezi ambalo litawaathiri watoto wetu kiakili na Hata kitaaluma.
 
nafikiri wanafuta ushahidi ili watakaobainika kukeketwa wahusika waliowafanyia hivyo wawapeleka kwa pilato
 
napata shida juu ya mechanism itakayotumika kuwapima will it use a certain device or free hand
 
Navyojua issue ya fgm ni mtambuka.ni kama kumwambia mtu aache imani yake.Ushauri wangu tuendelee kutoa elimu tu na tusitarajie big result now.Never.Unamwambiaje mtu aache kuruka na ungo usiku halafu ategemee eti ataacha?
 
mmmh, hawa jamaa sasa wameanza kwenda kinyume na ...., tunakoenda watapima hadi bikira kabla binti hajafungishwa ndoa.
 
Kweli serikali ya awamu hii imeamua ku deal na katerero tu.. njaa baadae.
 
1. Mbona simple tu vifaa vinavyotumika ni king'amuzi na Tv, sasa km ujuavyo normal HD decoder lazima iwe na high quality pics.

Kwa wale waliokatwa antennae zao huwezi kuona hata local channels.
 
WANAWAPIMA ILI WAWAFANYE NINI?
mi nikute mwanangu kafunuliwa in the name ya kupima waliokeketwa!
 
1. Mbona simple tu vifaa vinavyotumika ni king'amuzi na Tv, sasa km ujuavyo normal HD decoder lazima iwe na high quality pics.

Kwa wale waliokatwa antennae zao huwezi kuona hata local channels.
MSIFANYE MASIKHARA NA MAUMIVU YA WATU!
wapo watu wanashindwa kabisa kuwa na mahusiano kutokana na hii!
 
C:\Users\KAROLI\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.png

View attachment 457673

Hodi wanajamvi, Nimatumaini yangu yakwamba muwazima wa afya!!!!

Nina maswali machache juu ya mpango mkakati huu ambao uko mbioni kuwa implemented

1. Ni kifaa gani kitakacho tumika wakati wa kuwapima wanafunzi na human assistance itakayohusika itakuaje?

2. Kitendo cha kuwapima wanafunzi bila ridhaa yao kikoje hapa?

3. Side effect zitakaowapata waliokeketwa na wasiokeketwa limeangaliwaje hapo?

4. Je swala la kupima ndio njia pekee ya kumaliza tatizo la kukeketa watoto wa kike?

5. Kwa nini campaign isifanyike mikoa husika kuelimisha jamii kuliko kulenga watoto wa kike wasiokuwa na sauti kwa wazazi wao pindi maamuzi yaolewapo, wakati mikoa husika inajulikana bayana hapa nchini?

Nawasilisha karibuni kwa maoni yenu wanajamvi
Baada ya kufahamu waliokeketwa inakuwaje? Acheni kuendelea kudhalilisha wanawake, mmezidi sasa. muwakekete, halafu sasa mwende kuwachungulia tena, acheni upuuzi huu. Hivi kwa nini wanawake jamani???
 
Back
Top Bottom