Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,895
- 7,047
Ndugu wana JF, mara nyingi asubuhi nimekuwa nashuhudia wanafunzi tena wa umri mdogo wakiwa wanaongoza magari yanayopita karibu na maeneo ya shule zao. Naamini ni juhudi za walimu wa shule husika ili kuweza kulinda maisha ya wanafunzi wao.
Hata hivyo binafsi naamini kwamba askari wa usalama barabarani wapo wengi na hawawezi kushindwa kufanya kazi hiyo kwa nyakati zile za asubuhi wanafunzi wanapokuwa wanaingia shuleni na pia jioni wanapokuwa wanatoka. Sioni mantiki ya askari wengi kujazana pale round about ya Kigogo jijini Dar huku watoto wadogo kama hawa waliopo pichani wakiongoza magari katika shule ya msingi Rutihinda ambayo ipo hatua chache tu kutoka kwenye hiyo round about.