eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,355
- 16,402
Madrassa Zanyanyasa Wanafunzi Senegal
Wanafunzi 16 walifariki katika shule za masomo ya Qur'an, au madrasa, nchini Senegal kati ya mwaka 2017 na 2018 kutokana na mateso ya kupigwa, kutelekezwa au kunyanyaswa na walimu wao, kulingana na HRW
Human Rights Watch pamoja na muungano wa mashirika ya utetezi wa haki za binadamu nchini Senegal,
PPDH, wametoa ripoti hiyo ikieleza kwamba zaidi ya wanafunzi laki moja wanalazimishwa na walimu wao kwenda barabarani kuomba pesa na chakula na wamewekewa viwango vya pesa na vyakula wanavyofaa kufikisha na wasipofikisha wanadhibiwa.
Ripoti hiyo inaonyesha kwamba jumla ya wanafunzi 63 waliohojiwa miongoni mwa 88 walisema walimu wao wanawalazimisha kuomba na kwa siku wanafaa kuleta kuanzia dola senti 20 hadi dola mbili na senti ishirini. Zaidi, Mashirika hayo yaliwashuhudia baadhi ya wanafunzi walioteswa wakiwa wagonjwa, wakiwa na vidonda na makovu na hawajapokea matibabu.
Mwanafunzi wa Madrassa - Moussa, akiwa na karai ya kuoga katika kituo cha Maison de la Gare
kinachowakoa wanafunzi kutoka ombaomba barabarani
Wanafunzi hao wanaofahamika kwa jina la Thalib wanaripotiwa kuendelea kunyanyaswa ambapo mwezi Februari mwaka huu mwanafunzi mmoja alikuwa anazurura usiku katika kituo cha mabasi cha Saint-Louis akihofia kurudi madrassa kwa sababu hajafikisha kiwango cha fedha alichowekewa, mwanafunzi huyo pia aliwahi kunyanyaswa kimapenzi na mwanafunzi mwenzake wa umri wa makamo.
Mwezi wa nne mwalimu mmoja alikamatwa katika eneo la Mbour baada ya mwanafunzi kufariki kwa madai ya kupigwa.
Kuanzia umri wa miaka 5 wanalazimishwa kuombaomba
Thalib wa umri wa miaka 9 aliyehojiwa alisema hapendi Madrassa hizo kwa sababu wanapigwa kila wakati wasipohifadhi aya za Quran ama wasipoleta fedha, anasema wanapigwa hadi wanaona watafariki.