Wanafunzi Ardhi nao waanza mgomo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Wanafunzi Ardhi nao waanza mgomo
Thursday, 23 December 2010 20:08

Ibrahim Yamola na Imakulate Peter
MWAMKO wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kudai haki zao jana ulihamia Chuo Kikuu cha Ardhi ambako wanafunzi wameamua kuanza mgomo wakishinikiza serikali kumaliza kero kumi ikiwa ni pamoja na upungufu wa mabweni na vitambulisho, siku chache baada ya serikali kuridhia madai ya wenzao wa Dodoma.

Mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), ambao ulisababisha vurugu na uharibifu kabla ya serikali kusalimu amri, ulifuatiwa na mgomo wa wanafunzi wa Chuo cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chang'ombe (Duce) ambao walitulizwa kabla ya kuanza kugoma.

Jana wanafunzi wa Ardhi walianza kutekeleza uamuzi wao wa kugomea masomo baada ya Bunge la Wanafunzi kutoa baraka ya kutumia njia hiyo kuishinikiza serikali kutatua matatizo yao ambayo ni pamoja na kuondolewa kwa mkurugenzi wa shahada ya kwanza na mshauri wa wanafunzi kwa madai ya kuchelewesha kupeleka majina bodi ya mikopo na kufanya kazi za usajili badala ya kuwashauri wanafunzi.

Pamoja na kero hizo, wanafunzi hao pia wanataka kubadilishwa kwa vitambulisho, kuongezwa kwa mabweni, kumalizwa kwa tatizo la uhaba wa walimu na vifaa vya kujifunzia, upungufu wa vitabu na kuboreshwa kwa kantini za wanafunzi.
“Mazingira haya magumu yamesababisha baadhi ya wanafunzi wa kike kufanya matendo ya kikahaba na wanaume kufanya vutendo vya wizi ili kujipatia kipato,” alisema rais wa Serikali ya Wanafunzi (Aruso), Tegemeo Sambili.

Wanafunzi hao wanamtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda afike kuwatatulia kero zinazowakabili chuoni hapo na kwamba madai yao ya msingi ni pamoja na kero upungufu wa mabweni chuoni hapo inayowasababisha wengi wao kulala nje.
Akizungumzia kero hiyo, Sambili alisema baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu yanayowashawishi kujiingiza katika matendo yasiyofaa.

Sambili alisema wanafunzi wamekuwa wakichelewa kupata mikopo kutokana na uongozi kuchelewa kupeleka majina yao Bodi ya Mikopo na hivyo kusababisha waishi maisha ya shida kutokana na fedha kuchelewa kuwafikia.

“Kutokana na hayo wanafunzi wamechoshwa na utendaji kazi wa Dk Liwa kama mkurugenzi kwa kuwa amekuwa akisababisha matatizo mengi; amekuwa akichelewesha kupeleka majina kwenda Bodi ya Mikopo kutoka kwenye ofisi yake na kusababisha wanafunzi kuchelewa kupata pesa kwa wakati,” alisema Sambili.

Naye spika wa bunge la wanafunzi, Jikora Emmanuel alisema kuwa kukosekana kwa vitambulisho vya wanafunzi ni tatizo jingine linalowasumbua kila wakati na kuwa mpaka sasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawana vitambulisho wakati wale wa mwaka wa pili wamepewa vikarakasi tu.

“Uongozi wa chuo uliahidi kutoa vitambulisho vyenye hadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu lakini hadi sasa hakuna lolote lililofanyika. Wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawana kabisa na hivi sasa wana wiki saba tangu walipojiunga na chuo,” alisema Emmanuel.

Awali wanafunzi walimtaka makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Mshoro kufika na kuzungumza lakini hawakufanikiwa na ndipo walipoamua kufunga mlango wa jengo la utawala.

Profesa Mshoro alizungumza na wanafunzi baada ya kufika kwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana na kuwatuliza wanafunzi hao baada ya kufanya naye mazungumzo.

“Naombeni niende ndani nizungumze na mkuu wenu ili nijue matatizo yenu na namna ya kuwasaidia,” alisema Rugimbana.
 
Serikali ndio chanzo cha vurugu vyuoni Thursday, 23 December 2010 20:50

ardhi%20mgomo.jpg
KWA muda mrefu sasa wanafunzi katika baadhi ya vyuo vikuu nchini wamekuwa katika migomo ili kuishinikiza Serikali kusikiliza matatizo yao na kuyatafutia majibu. Hivyo, wamesema kwa kuwa mamlaka husika zimetia pamba masikioni, njia pekee iliyobaki ni kugoma, kwa maana ya kutoingia madarasani.

Ni kwa sababu hiyo tumeshuhudia habari za migomo katika vyuo hivyo zikitawala kurasa za vyombo vya habari katika muda wa wiki mbili zilizopita. Na katika kuchunguza kwa kina kuhusu kiini cha matatizo ya wanafunzi hao, moja ya mambo yanayojitokeza ni kuwa matatizo hayo yanafanana kwa kiasi kikubwa na karibu yote yanaelekezwa kwa Serikali.


Matatizo hayo yalianzia katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), ambapo wanafunzi wa chuo hicho walivamia ofisi za bodi inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HELSB), wakitaka bodi hiyo iwaongeze fedha ili kufidia kiwango cha ada iliyoongezwa na uongozi wa chuo hicho, lakini waliambiwa kuwasilisha malalamiko yao katika wizara husika. Wizara hiyo ilisalimu amri na kuahidi kumaliza matatizo yao.

abla vumbi la sakata la IFM halijatulia, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (Kampasi ya Tanzania), nao waliivamia wizara hiyo kuwasilisha madai yao kuhusu mikopo na kuambiwa kuwa Serikali ingechukua hatua kuhusu madai hayo. Na siku tano zilizopita, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), waligoma na kuzua tafrani kubwa iliyosababisha uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali, hatua iliyojibiwa na polisi ambao walivamia chuo hicho na kuwapiga wanafunzi kabla hawajaondoka na viongozi wa serikali ya wanafunzi na kuwasweka rumande.

Wanafunzi hao walikuwa wanaishinikiza Serikali iwalipe fedha za mafunzo kwa vitendo na kutengeneza miundombinu chuoni hapo ambayo ilikuwa katika hali mbaya, licha ya madai yao mengine ya kuwapo uhaba mkubwa wa maji na wahadhiri. Lakini katika hatua ya kushangaza, Serikali ilisalimu amri ambapo waziri husika, Shukuru Kawambwa na mwenzake wa mambo ya ndani, Shamsi Vuai Nahodha, pamoja na kuamuru kuachiwa huru kwa viongozi wa wanafunzi waliokamatwa na polisi, walikodi ndege na kukutana na wanafunzi hao usiku kucha katika chuo hicho, na hatimaye kuwatangazia kuwa Serikali imekubali kutatua matatizo yao baada ya kuyaona kuwa ni ya msingi.

Wakati Serikali ikihaha kutafuta suluhisho la matatizo ya Udom, jana wanafunzi wa Chuo cha Ardhi walianza rasmi mgomo wakiishinikiza Serikali itatue kero zao kumi, zikiwamo uhaba wa malazi kwa wanafunzi chuoni hapo na kushindwa kwa Serikali, kupitia bodi ya mikopo, kutangaza majina ya wanafunzi katika chuo hicho ambao watapewa mikopo. Uongozi wa chuo hicho unadai kuwa tayari umeipelekea bodi majina hayo wakati bodi hiyo inakana kupokea majina hayo.

Hiyo ndio hali halisi katika vyuo vyetu vya elimu ya juu hivi sasa, na huo ndio utendaji usiowajibika wa Serikali na vyombo vyake vinavyohusika moja kwa moja na kuhudumia wanafunzi hao. Ni dhahiri kuwa wanafunzi wameishika pabaya Serikali ambayo inaonekana kuwa haina pa kutokea, kwani wamechoshwa na ngonjera za ‘ufinyu wa bajeti ya Serikali' zinazoimbwa na vigogo wa serikali hiyo, huku wakiendelea kununua magari ya kifahari yenye gharama ya Sh280 milioni kila moja.

Kama hali ndio hiyo, tutegemee migomo zaidi katika vyuo vingine, kwani wanafunzi katika vyuo hivyo nao watataka watekelezewe madai yao kama Serikali ilivyoahidi kufanya katika vyuo vilivyogoma. Lakini kama tulivyosema katika safu hii siku chache zilizopita, matatizo mengi katika vyuo vingi nchini yanatokana na kukatika kwa mawasiliano kati ya wanafunzi na uongozi wa vyuo, bodi ya mikopo na wizara husika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom